Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi yaendayo kwa haraka (DART), Dkt.Edwin Muhede akizungumza na waandishi wa habari wakati akieleza mafanikio ya DART ndani ya mwaka mmoja wa Serikali ya Awamu ya Sita Madarakani.
Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji na Usimamizi wa miundombinu DART, Dkt.Philemon Mzee akizungumza na Waandishi wa Habari wakati DART ikieleza mafanikio ya DART ndani ya mwaka mmoja wa Serikali ya Awamu ya Sita Madarakani.Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Usafiri DART Mhandisi Fanuel Kalugendo akizungumza na Waandishi wa Habari wakati DART ikieleza mafanikio ya DART ndani ya mwaka mmoja wa Serikali ya Awamu ya Sita Madarakani. Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi yaendayo kwa haraka (DART), Dkt.Edwin Muhede akiwa pamoja na watumishiwa DART wakitembelea daraja la juu la Mabasi yaendayo haraka katika makutano ya barabara Uhasibu na Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam wakati akifanya ziara na waandishi wa habari kuangalia miundombinu ya barabara ya Mabasi yaendayo haraka awamu ya pili.Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi yaendayo kwa haraka (DART), Dkt.Edwin Muhede akizungumza mara baada ya kutembelea daraja la juu la Mabasi yaendayo haraka katika makutano ya barabara Uhasibu na Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam wakati akifanya ziara na waandishi wa habari kuangalia miundombinu ya barabara ya Mabasi yaendayo haraka awamu ya pili.
Daraja la juu la Mabasi yaendayo haraka katika makutano ya barabara Uhasibu na Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam ujenzi ukiendelea
(PICHA NA EMMANUEL MBATILO)
******************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi yaendayo kwa haraka (DART), Dkt.Edwin Muhede ameeleza maeneo ambayo Wakala hao inajivunia kufanya vizuri kwa kipindi cha mwaka mmoja wa Serikali ya Awamu ya Sita Madarakani.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Machi 12, 2022 katika mkutano maalum Dkt.Muhede amesema DART imefanya mambo mengi katika kuwatumikia Wananchi kwenye masuala ya usafiri ambapo katika hayo ina maeneo yaliyofanikiwa zaidi.
Amesema katika maendeleo ya ujenzi wa miundombinu ya usafiri katika mwaka mmoja wa Serikali ya awamu ya Sita wamefanikiwa kukamilisha ujenzi wa karakana ya ubungo hivyo kuwa msaada wa karakana ya Jangwani.
Aidha amesema katika ujenzi wa miundombinu ya awamu ya pili ambao unajumuisha barabara ya Kilwa, tawi la barabara ya Kawawa yenye jumla ya kilometa 20.3.
"Ujenzi kwa awamu ya pili unafanywa kwa mafungu mawili, fungu la kwanza ni ujenzi wa barabara na vituo vya mabasi katikati ya barabara kuu ya Kilwa, fungu la pili ni ujenzi wa majengo yaani vituo mlisho Karakana na vituo vikuu ". Amesema Dkt.Muhede.
Ameeleza kuwa hatua iliyofikia kwenye ujenzi fungu la kwanza ni asilimia 50.07% hadi kufikia machi 2022 ikilinganishwa na asilimia 11.82% machi 2021.
Hata hivyo amesema maendeleo ya ujenzi wa fungu la pili umekamilika kwa asilimia 100% hasi kufikia machi 2022 ikilinganishwa na asilimia 88%machi 2021.
0 Comments