Ticker

6/recent/ticker-posts

DC IRAMBA AOMBA KUANDIKWA UPYA HISTORIA YA WAPIGANIA UHURU NCHINI



Mkuu wa Wilaya ya Iramba mkoani Singida Suleiman Mwenda akisalimiana na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Innocent Msengi baada ya kuwasili kwenye maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambayo Kiwilaya yalifanyika katika Kijiji cha Kyalosangi wilayani humo jana.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Innocent Msengi, akizungumza kwenye maadhimisho hayo.
Mkuu wa Wilaya ya Iramba mkoani Singida Suleiman Mwenda, ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye sherehe hiyo akihutubia. Kutoka kushoto ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Taifa ya Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Mwalimu Shani Ulumbi, Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya hiyo, Monica Samwel, Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Wilaya ya Iramba, Rydia Kidaila na Katibu wa UWT, Catherine Sarwat.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Iramba, Samwel Ashery akizungumza kwenye hafla hiyo.
Katibu wa CCM Wilaya ya Iramba, Ephrahimu Kolimba akizungumza kwenye sikukuu hiyo.

Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Taifa ya Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Mwalimu Shani Ulumbi akizungumza kwenye sherehe hiyo.
Viongozi wakiwa kwenye sherehe hizo. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya hiyo, Samwel Ashery, Katibu wa CCM, Ephrahim Kolimba na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Innocent Msengi.
Diwani wa Tarafa ya Kinampanda, Hidaya Msangia akifungua sherehe hizo.
Sherehe zikiendelea.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Michael Matomora (kulia) akikagua bidhaa za wajasiriamali waliohudhuria sikukuu hiyo.

Sherehe zikiendelea.
Viongozi wanawake kutoka idara mbalimba wilayani humo wakifurahi wakati wakisubiri kumpokea mgeni rasmi Mkuu wa wilaya hiyo, Suleiman Mwenda.
Wanafunzi wa Shule ya Wasichana ya Tumaini Kinampanda wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
Mgeni rasmi wa sherehe hizo Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda akipata maelezo kutoka kwa wajasiriamali wakati alipokuwa akitembelea mabanda yao.
Mgeni rasmi wa sherehe hizo Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Suleiman Mwenda akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Tawi la NMB Kiomboi, David Diwi (wa pili kulia).
Utembeleaji wa mabanda ukiendelea.
Afisa Tarafa ya Kinampanda, Cholo Mtaki akiwatambulisha viongozi kwenye hafla hiyo.
Wanakwaya waKikundi cha Upendo B wakitoa burudani kwenye sherehe hizo.
Madansa kutoka Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Tumaini wakiupiga mwingi kwenye sherehe hizo.
Watoto kutoka Shilo Student Centre wakitoa burudani.
Wanawake wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba wakiwa kwenye hafla hiyo.
Wanawake wa Wilaya ya Iramba wakiserebuka.
Vijana wa Skauti wakiwajibika kwenye sherehe hiyo.
Sherehe ikiendelea.
Wanafunzi wakiwa kwenye maadhimisho ya sikukuu hiyo.
Baadhi ya Walimu kutoka Chama cha Walimu (CWT) wilayani humo wakitoa msaada wa vitu mbalimbali kwa wagonjwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kiomboi ikiwa ni moja ya shughuli ya maadhimisho hayo.
Msaada ukitolewa.
Picha ya pamoja kabla ya kukabidhi msaada huo.



********************


Na Dotto Mwaibale, Iramba



MKUU wa Wilaya ya Iramba mkoani Singida Suleiman Mwenda ameiomba Serikali kuandika upya historia ya wapigania Uhuru nchini ili kutoa fursa ya kuigizwa kwa wapigania Uhuru wanawake ambao nao walifanyakazi kubwa ya kupigania uhuru lakini kwenye historia hawakujumuishwa.

Mwenda alitoa ombi hilo jana katika maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani ambayo yalifanyika Kiwilaya katika Kijiji cha Kyalosangi wilayani humo na kusisitiza kuwa kuandikwa kwa historia upya ya wapigania Uhuru itasaidia kwa kiasi ki kubwa vizazi vya sasa na vijavyo kujua jinsi wanawake walivyo shiriki kikamilifu katika kutafuta uhuru wa Tanzania.

Akimtolea mfano wa mmoja wa mwasisi Mwanamke aliyejitoa kwa hali na mali katika kupigania Uhuru wa Tanzania Khadija Kamba ambaye hajawahi kuandikwa sehemu yoyote kwenye historia ya wapigania Uhuru Mwenda alisema waasisi hawa historia yao inapaswa kuandikwa kwa faida ya Taifa letu.

Alimtaja mwasisi mwingine kuwa ni Mke wa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, Mama Maria Nyerere ambaye wakati mume wake alipoacha kazi ya kufundisha na kuanza harakati za kupigania uhuru yeye alifungua duka maeneo ya Kariakoo ambapo alikuwa akiuza mafuta ya taa na kupata fedha za kuendeshea maisha yao.

“Mama Nyerere kwa namna moja hama nyingine anaingia katika historia hiyo licha ya kwamba naye hajaandikwa mahali popote katika ushiriki wake wa kupigania nchi hii” alisema Mwenda.

Akizungumzia kuhusu vitendo vya ukatili kwa wanawake alisema katika wilaya hiyo bado kuna baadhi ya jamii zinaendelea kukumbatia mila potofu ikiwemo ya kuwanyima mirathi wanawake wajane jambo ambalo linatakiwa kukomeshwa katika jamii.

“Sisi kama Serikali katika ngazi ya wilaya tumeendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuhakikisha tunaziondoa mila zote potofu na kandamiz” alisema Mwenda.

Aidha Mwenda alisema wilaya hiyo imekomesha vitendo vya ukeketaji wawanawake na wasicha kutokana na kuimarishwa kwa utoaji wa elimu kuhusu madhara ya ukeketaji katika jamii.

Alisema kazi iliyofanyika na kukomesha vitendo hivyo wilayani humo ni kubwa ambapo ameitaka jamii kutorudi nyuma na kurudia vitendo hivyo ambayo vinadhalilisha utu wa mtu.

Katika hatua nyingine alisema Halmashauri hiyo kupitia mikopo inayotolewa kutoa asilimia 10 ya mapato ya ndani kwa mwaka 2020/2021 jumla ya Sh.59,758,624.39 ilitolewa katika vikundi tisa vya wanawake ambapo pia kwa mwaka 2021/2022 jumla ya Sh.17,301,745.70 zilitolewa katika vikundi vitatu vya wanawake na kuwa jumla ya vikundi 12 vilivyopata mkopo wenye jumla ya Sh.77,060,370.09.

“Leo hii tunapoadhimisha maadhimisho haya Halmashauri inatoa mikopo kwa vikundi viwili vya wanawake ambavyo ni Kikundi cha Tumaini kilichopo Kijiji cha Tyeme Kata ya Mtoa ambacho kinapewa mkopo wa Sh.20,000,000 na kikundi cha Nansule kilichopo Kijiji cha Ntwike ambacho kinapewa Sh.7,520,000 na kufanya jumla ya vikundi vyote vya wanawake vilivyopewa mkopo kuanzia mwaka 2020/2021 hadi mwaka 2021/ 2022 kufikia vikundi 14 vilivyopewa mkopo wenye thamani ya jumla ya Sh.104,060,370.9.

Akisoma risala ya maadhimisho hayo yaliyokuwa na kauli mbiu isemayo “Kizazi cha Haki na Usawa kwa Maendfeleo Endelevu” Msoma Sara Mitula alisema jamii inapaswa kutambua kuwa maendeleo endelevu ni lazima yahusishe jinsia zote kwa kuzingatia haki na usawa ili kukuza uchumi wa jamii na Taifa kwa ujumla.

Alisema kauli mbiu hiyo inakinzana na hali halisi iliyopo katika jamii kutokana na kuwepo kwa mfumo dume kwa baadhi ya makabila hali inayopelekea wanawake kuonekana kuwa ni viumbe dhaifu ambao hawawezi kuwa na maamuzi yoyote katika familia na jamii kwa ujumla.

Alisema Mila na desturi kandamizi nayo ni sababu moja wapoinayo mfanya mwanamke kutopewa fursa sawa na mwanaume hususani katika suala zima la Elimu kwani familia na jamii kwa ujumla humpa kipaumbele mtoto wa kiume kuliko wa kike.

Mitula alitaja mambo mengine kuwa ni kukosekana kwa fursa ya kumiliki mali, na usawa katika suala zima la mirathi.

Katika kuadhimisha maadhimisho hayo kwa kushirikiana na Afisa Maendeleo ya Jamii wa wilaya hiyo, Jane Ng’ondi, Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Wilaya ya Iramba walitembelea Hospitali ya Wilaya ya Kiomboi na kufanya matendo ya huruma kwa kutoa vitu mbalimbali kwa wagonjwa katika wodi ya wajawazito na wazaza kama sabuni, maji, mafuta na vingine vingi.

Akizungumza na wagonjwa hao wakati wa kukabidhi msaada huo Mwalimu Verian Masanja kutoka Kitengo KE Chama cha Walimu wilayani humo alisema wanaungana na wanawake wote hapa nchini na duniania kwa ujumla katika kusherehekea sikukuu hiyo na kuwa wanaziunga jitihada zinazofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan za kuwaletea wananchi maendeleo.

Post a Comment

0 Comments