Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji, Viwanda, Biashara na Mazingira Mhe. David Kihenzile akizungumza wakati wa kikao na Kamati ya kusimamia Afisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa ya Baraza la Wawakilishi leo Machi 17, 2022 katika ukumbi wa Ofisi za Baraza la Wawakilishi, Chukwani, Zanzibar kwa lengo la kufahamiana na kubadilishana uzoefu katika masuala ya uhifadhi wa mazingira.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis aliyeambatana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji, Viwanda, Biashara na Mazingira akifafanua jambo wakati wa ziara kukutana na Kamati ya kusimamia Afisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa ya Baraza la Wawakilishi leo Machi 17, 2022, kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi za Baraza la Wawakilishi chukwani.
Makamu wa Mwenyekiti wa Kamati ya kusimamia Afisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa ya Baraza la Wawakilishi, Mhe. Mtumwa Pea Yussuf akizungumza wakati kamati yake ilipokutana na kubadilishana uzoefu kuhusu masuala ya hifadhi ya mazingira na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji, Viwanda, Biashara na Mazingira katika ukumbi wa Ofisi za Baraza la Wawakilishi, Chukwani, Zanzibar leo Machi 17, 2022.
Sehemu ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji, Viwanda, Biashara na Mazingira pamoja na wataalamu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais walioambatana na kamati hiyo wakiwa katika kikao na Kamati ya kusimamia Afisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa ya Baraza la Wawakilishi leo Machi 17, 2022 katika ukumbi wa ofisi za Baraza la Wawakilishi Chukwani, Zanzibar.
Mkurugenzi wa Mazingira kutoka Afisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Bi. Farhat Mbarouk akifafanua jambo wakati wa kikao cha kubadilishana uzoefu kati ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji, Viwanda, Biashara na Mazingira na Kamati Kamati ya kusimamia Afisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa ya Baraza la Wawakilishi leo Machi 17, 2022 katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi, Zanzibar.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji, Viwanda, Biashara na Mazingira, wataalamu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais walioambatana na kamati hiyo wakiwa katika kikao cha kubadilishana na uzoefu kuhusu masuala ya hifadhi ya mazingira picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ya kusimamia Afisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa ya Baraza la Wawakilishi mara baada ya kufanyika kwa kikao kati yao leo Machi 17, 2022 katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi, Zanzibar.
(PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS)
**************************
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji, Viwanda, Biashara na Mazingira imefanya ziara Zanzibar na kukutana na Kamati ya kusimamia Afisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa ya Baraza la Wawakilishi leo Machi 17, 2022 katika ukumbi wa Ofisi za Baraza la Wawakilishi uliopo Chukwani.
Katika ziara hiyo kamati iliambatana na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis, Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Bw. Edward Nyamanga na wataalamu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais.
Akizungumza wakati wa kikao hicho Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji, Viwanda, Biashara na Mazingira Mhe. David Kihenzile alisema ziara hiyo inalenga kukagua miradi ya mazingira inayotekelezwa na Ofisi ya Makamu wa Rais.
Pia Mhe. Kihenzile alisema kuwa wajumbe wa kamati yake wanakutana na kamati hiyo kwa lengo la kufahamiana na kujitambulisha kwa vile kamati hizo mbili zina majukumu ya kuisimamia Serikali katika sekta ya mazingira.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis alisema kuwa ziara ya kamati hiyo pamoja na wataalamu inalenga kukagua miradi ya kimazingira.
Mhe. Khamis alisema kuwa suala la mazingira hususan katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi linagusa Serikali zote mbili yaani Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ).
Alisema kuwa kutokana na changamoto hizo za kimazingira Serikali hizi mbili zinafanya jitihada za dhati katika kukabiliana nazo.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya kusimamia Afisi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa ya Baraza la Wawakilishi Mhe. Mtumwa Pea Yussuf alisema kamati yake inasimamia wizara nne ikiwemo Ofisi ya Makamu wa Rais (inayoratibu masuala ya mazingira), Ofisi ya Makamu wa Pili, Tawala za Mikoa pamoja na Wizara ya Katiba na Sheria.
Alipongeza jitihada za Serikali katika kushughulikia changamoto za kimazingira zinazoyakabili maeneo mbalimbali ya Unguja na Pemba zikiwemo ujenzi wa kuta za kupunguza mwimbi ya bahari katika ukanda wa Pwani ya Bahari ya Hindi.
Mhe. Mtumwa alitoa rai kwa Serikali kuongeza kasi ya kutatua changamoto za mabadiliko ya tabianchi zikiwemo huku akionesha wasiwasi wake kuhusu baadhi ya visiwa kuliwa na maji ya bahari na kupendekeza kamati hizi kutoka pande mbili za Muungano kushirikiana ili kunusuru mazingira.
0 Comments