************************
Na. Dominic Haule
Kituo Cha Sheria na Utetezi haki za Binadamu LHRC kimetoa Mapendekezo kwa kikosi kazi Cha kuratibu Maoni ya Wadau ikiwemo ni kufanyika mikutano ya hadhara kwa vyama vyote pamoja na Jeshi la Polisi kutoingilia Maswala ya Uchaguzi.
Mapendekezo hayo ametoa leo Jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mtendaji Bi Anna Henga Wakati akizingumza na Waandishi wa Habari ofisi kwao iliyopo kijitonyama
Amesema kuwa kituo kina Imani kuwa kikosi kazi kitazingatia maoni yaliyo tolewa na Wadau mbalimbali katika Mchakato wa kupata sheria mpya ya Usimami wa Uchaguzi..
Wakati huo huo ametoa wito kwa kwa Kikosi Cha wadau wa Demokrasia na Utawala Bora kuhakikisha wanazingatia misingi iliainisha katika mkataba Afrika wa Demokrasia na la Utawala 2017 wa vyama vya kiasiasa.
Aidha kituo cha haki za Binadamu kitaendelea kutoa Ushirikiano kwa kikosi kazi pale itakapo hitajika ili kuhakisha wanafikia malengo ya pamoja ya kuwa na sheria ilio sawa na kuwa na ya kuleta Uchaguzi wa haki na uhuru pale unapofanyika hapa Nchini Tanzania.
0 Comments