Ticker

6/recent/ticker-posts

MAANDALIZI YA UFUNGUZI WA DARAJA LA TANZANITE KESHO YAMEKAMILIKA 95%


Mkuu wa Itifaki Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Yusuf Mndolwa Tindi kulia akizungumza na Bw. Gibson Mwaya Afisa Sayansi ya Jamii Mkuu Wakala wa Barabara TANROARDS katikati mara baada ya kukagua maandalizi ya eneo litakalotumiwa kwa ajili ya hafla ya uzinduzi wa daraja la Tanzanite ilnalokatisha baharini eneo la Sea View Upanga kuelekea Oysterbay jijini Dar es Salaam ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuweka historia nyingine kwa kulifugua rasmi daraja hilo lenye urefu wa kilometa 1.03 pamoja na barabara unganishi zenye urefu wa kilomita 5.2.

..................................................

Maandalizi ya eneo litakalotumiwa kwa ajili ya hafla ya uzinduzi wa daraja la Tanzanite linalokatisha baharini eneo la Sea View Upanga kuelekea Oysterbay jijini Dar es Salaam ambalo kesho Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuweka historia nyingine kwa kulifugua rasmi daraja hilo lenye urefu wa kilometa 1.03 pamoja na barabara unganishi zenye urefu wa kilomita 5.2 yamekamilika kwa asilimia 95.

Akizungumza na Mtandao wa Fullshangweblog jioni hii Bw. Gibson Mwaya Afisa Sayansi ya Jamii Mkuu Wakala wa Barabara TANROARDS amesema kila kitu kinakwenda sawa na maandalizi yamekamilika kwa kiasi kikubwa.

Mwaya ameongeza kuwa Rais Samia Suluhu Hassan anakwenda kuandika historia kwa watanzania kwa kufungua rasmi daraja hilo ambalo lilianza kujengwa mwaka 2018 baada ya aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya tano Hayati Dk. John Pombe Magufuli kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya kuanza kwa ujenzi huo.

Amesema kwamba sherehe hiyo itakuwa ni kubwa na itakuwa ni fursa kwa watanzania kuona yale yaliyoahidiwa na serikali yao yametekelezwa ambapo tayari tumeruhusu magari yaanze kupita toka mwezi wa pili mwaka huu.

Bw. Mwaya amewakaribisha wananchi wa mkoa wa maeneo mbalimbali kufuatilia kwenye vyombo mbalimbali vya habari ili kujionea tukio hilo moja kwa moja kupitia luninga na mitandao ya kijamii.


Bw. Gibson Mwaya Afisa Sayansi ya Jamii Mkuu Wakala wa Barabara TANROARDS kulia akimsikiliza Mhandisi Mwanaisha Rajabu Mhandisi Miradi wa Mkoa wa Dar es Salaam TANROARDS wakati wakijadiliana jambo katika maandalizi hayo.


Baadhi ya maofisa kutoka wilzara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakijadiliana jambo wakati wakiwa katika shughuli nzima ya maandalizi ya uzinduzi wa Daraja hilo.


Bw. Gibson Mwaya Afisa Sayansi ya Jamii Mkuu Wakala wa Barabara TANROARDS kulia akielekeza jambo wakati wa maandalizi hayo.


Picha mbalimbali zikionesha maeneo majukwaa mbalimbali yakiendelea kupambwa na kuwekwa zawa kwa ajili ya uzinduzi wa Daraja la Tanzanite ambalo kesho Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kulifungua rasmi.

Post a Comment

0 Comments