Ticker

6/recent/ticker-posts

MAVUNDE AHIMIZA WATAFITI KUTATUA CHANGAMOTO ZA VISUMBUFU KWA WAKULIMA WA PAMBA


******************

Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. Anthony Mavunde amewataka watafiti kuongeza kasi ya kutoa elimu kwa wakulima juu ya mbinu sahihi za kudhibiti visumbufu kwenye zao la pamba pamoja na kuhakikisha wanalifanyia kazi suala la wadudu visumbufu waliovamia zao la pamba ambao wanaweza kupelekea kushuka kwa uzalishaji wa pamba kama hatua madhubuti hazitachukuliwa mapema.

Mh.Mavunde ameyasema hayo leo tarehe 18 Machi, 2022 Wilayani Misungwi, Mwanza alipotembelea Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha TARI Ukiriguru.

"Mmenionesha hapa namna mnavyofanya tafiti za kupambana na visumbufu kwenye zao la pamba, lakini dawa hizo hizo mlizotumia ndizo zinazolalamikiwa na wakulima kuwa hazifanyi kazi wanapozitumia kwenye mashamba yao, hivyo wekeni mkakati wa kutoa elimu kwa wakulima juu ya taratibu sahihi za unyunyiziaji wa viuatilifu kwenye mashamba yao pamoja na kufanya uchunguzi kwa kushirikiana na Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu(TPHPA) juu ya aina ya viuatilifu vinavyotumika na ubora wake katika kutatua changamoto hii ya athari kwa pamba ya wakulima.

Suala la tija kwa mkulima si la mbegu bora na kanuni za kilimo bora pekee, tusipodhibiti visumbufu tutakuwa hatuwasaidii wakulima kuweza kufikia tija kubwa ya uzalishaji na kuongeza kipato kutokana na pamba wanayozalisha.

Post a Comment

0 Comments