******************
NA EMMANUEL MBATILO
KLABU ya Yanga imeendelea kuusogelea ubingwa wa ligi ya NBC mara baada ya leo kuichapa Geita Gold 1-0 kwenye dimba la CCM Kirumba Jijini Mwanza.
Fiston Mayele ameendelea kuwatesa makipa wa ligi kuu ambapo leo tena kaweka kambani goli la pekee lililowapa pointi tatu muhimu kwenye ligi hiyo.
Mayele alifunga bao la mapema kabisa baada ya kuwashinda mabeki wa Geita Gold na kuweza kukwanjuka shuti kali lililomshinda kipa wa Geita Gold.
Mechi hii ambayo ilikumbwa na faulo nyingi kwa pande zote mbili na kusababisha wachezaji baadhi kutolewa nje kwa majeruhi.
0 Comments