**********************
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde leo amefanya ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo katika Kata ya Mkonze,Jijini Dodoma.
Maeneo yaliyotembelewa yanahusisha;
A. UKAGUZI WA DARAJA LA NZINJE Daraja hili ni sehemu ya Fedha zilizotolewa na serikali ya Mh Rais Samia Suluhu Hassan kwa majimbo yote nchini kuboresha miundombinu yake.
Ujenzi wa daraja umefikia zaidi ya asilimia 85 kukamilika kwake kutasaidia kuchochea shughuli za kiuchumi katika eneo la nzinje na upatikanaji wa huduma bora za kijamii.
B. UKAGUZI WA SHULE SHIKIZI
Shule hii inajengwa kwa nguvu za wananchi kwa lengo kubwa la kuwapunguzia mwendo wanafunzi wa eneo la nzinje kutotembea umbali mrefu kufuata shule ya Msingi Michese ilipo.
Mbunge Mavunde ameunga mkono juhudi za wananchi kwa kuchangia tofali 1000 za ujenzi wa madarasa.
3. UKAGUZI WA ENEO LA MRADI WA MASHAMBA YA MIJINI
Kufuatia kukamilika kwa Mpango kabambe (Master Plan) ya Jiji la Dodoma,baadhi ya maeneo yametengwa kwa ajili ya kilimo cha mijini ikiwemo eneo la nzinje ambapo taratibu za umilikishwaji wa mashamba kwa wananchi zimefikia hatua za mwisho ili wananchi wote wa eneo waweze kumiliki maeneo hayo kwa hati za umiliki wa ardhi.
0 Comments