Ticker

6/recent/ticker-posts

MBUNGE WA ULANGA SALIM ALAUDIN HASHAM ATOA BIMA ZA AFYA KWA WATOTO YATIMA NA KUKARABATI JENGO LAO KWA THAMANI YA MIL 15.5.

MBUNGE wa Jimbo la Ulanga Mkoani Morogoro Mhe. Salim Alaudin Hasham kulia akigawa kadi za bima ya afya.
MBUNGE wa Jimbo la Ulanga Mkoani Morogoro Mhe. Salim Alaudin Hasham kulia akigawa kadi za bima ya afya.
MBUNGE wa Jimbo la Ulanga Mkoani Morogoro Mhe. Salim Alaudin Hasham kulia akigawa kadi za bima ya afya kwa watoto yatima wanaoishi kwenye mazingira magumu 74wanaolelewa katika kituo cha Ukwama wilayani humo.
MBUNGE wa Jimbo la Ulanga Mkoani Morogoro Mhe. Salim Alaudin Hasham kulia akigawa kadi za bima ya afya kwa watoto yatima wanaoishi kwenye mazingira magumu 74wanaolelewa katika kituo cha Ukwama wilayani humo.
MBUNGE wa Jimbo la Ulanga Mkoani Morogoro Mhe. Salim Alaudin Hasham akiwa amembeba mmoja ya watoto wanaolelewa kwenye kituo hicho.
MBUNGE wa Jimbo la Ulanga Mkoani Morogoro Mhe. Salim Alaudin Hasham akiwa kwenye picha ya pamoja na watoto yatima wanaoishi kwenye mazingira magumu 74wanaolelewa katika kituo cha Ukwama wilayani humo mara baada ya kuwakabidhi kadi za bima ya afya.
MBUNGE wa Jimbo la Ulanga Mkoani Morogoro Mhe. Salim Alaudin Hasham kushoto akiteta jambo na mmoja wa wazee mara baada ya kugawa kadi za bima ya afya kwa watoto yatima wanaoishi kwenye mazingira magumu 74wanaolelewa katika kituo cha Ukwama wilayani humo.
MBUNGE wa Jimbo la Ulanga Mkoani Morogoro Mhe. Salim Alaudin Hasham akiwa kwenye picha ya pamoja na watoto yatima wanaoishi kwenye mazingira magumu 74wanaolelewa katika kituo cha Ukwama wilayani humo mara baada ya kuwakabidhi kadi za bima ya afya.
MBUNGE wa Jimbo la Ulanga Mkoani Morogoro Mhe. Salim Alaudin Hasham akiomba dua na watoto hao.
MBUNGE wa Jimbo la Ulanga Mkoani Morogoro Mhe. Salim Alaudin Hasham katika akiteta na Katibu wake Thomas Machupa kushoto mara baada ya kuwakabidhi kadi za bima ya Afya watoto yatima wanaoishi kwenye mazingira magumu 74wanaolelewa katika kituo cha Ukwama wilayani humo mara baada ya kuwakabidhi kadi za bima ya afya.
MBUNGE wa Jimbo la Ulanga Mkoani Morogoro Mhe. Salim Alaudin Hasham kulia akionyeshwa kitu na Katibu wake Thomas Machupa kushoto.

*****************

MBUNGE wa Jimbo la Ulanga Mkoani Morogoro Mhe. Salim Alaudin Hasham amewakatia bima za Afya watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu 74 wanaolelewa katika kituo cha Ukwama wilayani humo.


Akizungumza baada ya kugawa bima hizo Mhe Salim Alaudin ambaye pia ndie mlezi wa kituo hicho amesema lengo kubwa la kufanya zoezi hilo ni kuwahakikishia uhakika wa kupata matibabu kwa haraka bila Changamoto zozote ili kuwapunguzia mzigo Mkubwa wasimamizi wa kituo hicho.


Mbali na kuwakatia bima za Afya pia Mhe Salim Alaudin amefanya marekebisho ya Jengo wanaloishi watoto hao na kuwajengea vyoo bora ili mazingira yawe salama zaidi nanyakuvutia na watoto hao wasijisikie upweke kwa kipindi chote watakachoishi hapo.


Aidha Mhe Salim Alaudin ameongeza kuwa ukarabati wote huo utagharimu kiasi cha Shilingi Milioni 15.5 na fedha zote hizo zinatoka mfukoni mwake pia ataendelea kukisimamia kituo hicho ili kuhakikisha usalama na mazingira bora yanapatikana kwa watoto hao.


Kwa upande wake Msimamizi wa kituo hicho Bi. Redepta Choma amemshukuru Mbunge Salim Alaudin kwa moyo wake wa kujitoa kukisaidia kituo kwani ni watu wachache wanaoweza kufanya hivyo na amemuomba asichoke kuwasaidia na Mungu atambariki.


Redepta pia ameongeza kuwa zipo changamoto nyingi zilizokuwa zinawakabili awali ikiwemo huduma za Afya lakini kwasasa mlezi wao amejitahidi kuzipunguza kwa kiasi kikubwa.


Mama mlezi wa kituo hicho Bibi Elizabeth Choma amesema anamshukuru Mungu kwa kumleta Baba mlezi wao kwani walikuwa na hali mbaya lakini kwasasa Baba mlezi anawapambania na wanaona baadhi ya Changamoto Sinai soka taratibu.


Kituo hicho cha kulea watoto yatima na wenye mahitaji maalum UKWAMA kilianzishwa mwaka 1976 na kanisa katoliki kwa lengo la kuwasaidia wahitaji hususani watoto.

Post a Comment

0 Comments