Ticker

6/recent/ticker-posts

RAIS DKT.HUSSEIN MWINYI AWASILI MKOANI GEITA KUHUDHURIA KUMBUKIZI YA HAYATI MAGUFULI.


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi akisalimiana na Viongozi wa Serikali na Chama wa Mkoa wa Geita alipowasili Uwanja wa Ndege wa Chato,kwa ajili ya kuhudhuria Siku ya Kumbukizi ya Mwaka mmoja tangu kufariki kwa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli, inayofanyika leo 17-3-2022 Wilayani Chato .(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi (kulia kwa Rais) baada ya kuwasaili katika Uwanja wa Ndege wa Chato Mkoani Geita na (kushoto kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Rosemary Senyamule.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Mjane wa Marehemu aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli Mama Janeth Magufuli alipowasili katika Uwanja wa Magufuli Chato, kuhudhuria Siku ya Kumbukizi ya Mwaka mmoja tangu kufariki kwa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli, inayofanyika leo 17-3-2022 Wilayani Chato .(Picha na Ikulu)

Post a Comment

0 Comments