Ticker

6/recent/ticker-posts

RAIS SAMIA AAGIZA NEMBO YA DARAJA LA TANZANITE IBADILISHWE


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiondoa kitambaa pamoja na Balozi wa Korea hapa nchini Kim Sun Pyo kuashiria ufunguzi rasmi wa Daraja la Tanzanite lenye urefu wa Kilometa 1.03 pamoja na Barabara zake unganishi zenye urefu wa Kilometa 5.2 kuanzia eneo la Agha Khan (Barack Obama Road) hadi eneo la Coco Beach Jijini Dar es Salaam.

................................................

RAIS Samia Suluhu Hassan, amezindua daraja jipya la Selender (TANZANITE), lenye urefu wa kilomita 1.03 ambalo limetumia sh.bilioni 243 na kuagiza nembo ya mwenge wa uhuru iondolewe na kuwekwa ya Tanzanite

Akizungumza katika ufunguzi huo amesema nembo ya daraja hilo ibadilishwe kwa kutoa ya mwenge na kuwekwa ya Tanzanite ambayo italeta maana halisi ya jina kuhakikisha jiji hilo linakuwa la kisasa na kufungua fursa za kiuchumi na baishara.

Amesema, serikali itahakikisha inaendeleza miradi ya miundombinu ili kumaliza kero ya msongamano katika jiji la Dar es Salaam kwa kufanya upanuzi wa barabara na ujenzi wa barabara za juu.

Ameongeza kuwa miradi hiyo ikikamilika kero ya msongamano wa magari jijini humo itapungua na kuwa kichocheo kikubwa cha uchumi na biashara

“Maandalizi yanaendelea kwa ajili ya awamu ya tatu ya ujenzi wa barabara za mwendokasi kutoka katikati ya jiji hadi Gongolamboto,awamu ya nne kutoka katikati ya jiji hadi tegeta na awamu ya tano kutoka bandarini hadi Nelson Mandela, Kigogo hadi Tabata dampo na Segerea, Moroco, Kawe hadi Lugalo,”amesema.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Rogatus Mativila amesema kutokana ukuaji wa jiji hilo, ongezeko la watu na msongamano wa magari katika barabara ya Alhasan Mwinyi katika daraja la zamani la Selender, serikali iliona haja ya kujenga daraja hilo ambapo utafiti ulionyesha magari 52,000 yanapita katika eneo hilo.

Amesema daraja hilo limejengwa kwa ushirikiano kati ya serikali ya Tanzania kwa fedha za mkopo nafuu wa benki ya Exim ya Korea kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Kiuchumi wa nchi hiyo.

“Viwango vya usanifu wa daraja lina urefu wa kilomita 1030 sawa na KM 1.03 na upana wa mita 20.5 njia nne za magari na njia mbili za waenda kwa miguu na barabara unganishi za lami za njia nne zenye km 5.2 zenye upana sawa 5.2 zenye upana sawa na daraja ambazo ni barabara ya Kenyata yenye urefu mita km 500, Tule hadi njiapanda ya Chole kilomita 2.945, barabara ya Ufukweni inayounganisha Alhasan Mwinyi inayounganisha Barack Obama yenye uyenye urefu wa kilomita 325 na Ocean Road kilimita 1.2 na mpya ya daraja eneo la hospitali ya Agakhan urefu wa mita 680,”amesema.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa, Mtendaji Mkuu wa TANROADS Eng. Rogatus Mativila pamoja na viongozi wengine wa Serikali baada ya ufunguzi rasmi wa Daraja la Tanzanite lenye urefu wa Kilometa 1.03 pamoja na Barabara zake unganishi zenye urefu wa Kilometa 5.2 kuanzia eneo la Agha Khan (Barack Obama Road) hadi eneo la Coco Beach Jijini Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiakiongozana na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mh. Profesa Makame Mbarawa, Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Bw. Amos Makalla na Mwakilishi wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Mh. Miraji Mtaturu wakikagua daraja jipya laTanzanite mara baada ya uzinduzi huo leo.

Mtendaji Mkuu wa TANROADS Eng. Rogatus Mativila akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.


Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mussa Azan Zungu akizungumza katika uzinduzi huo.


Mwakilishi wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu Mh. Miraji Mtaturu


Baadhi ya viongozi wa dini wakijumuika katika uzinduzi huo.


Baadhi ya wananchi waliohudhuria katika uzinduzi huo


Baadhi ya wafanyakazi wa TANROADS pamoja na wananchi mbalimbali wakishiriki katika uzinduzi huo.


Picha mbalimbali zikionesha Mtendaji Mkuu wa TANROADS Eng. Rogatus Mativila akisalimiana na wafanyakazi mbalimbali wa TANROADS katika uzinduzi huo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.


Mtendaji Mkuu wa TANROADS Eng. Rogatus Mativila akisalimiana na wakandarasi waliojenga daraja hilo kutoka Korea Kusini ambao pia wamehudhuria katika uzinduzi huo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.


Picha mbalimbali zikionesha Msafara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanania Mh. Samia Suluhu Hassan ukipita kwenye daraja la Tanzanite pamoja na barabara zake unganishi wakati Mh. Rais alipokagua barabara hizo baada ya ufunguzi rasmi

Post a Comment

0 Comments