Ticker

6/recent/ticker-posts

RAIS SAMIA AFANYA MAMBO MAKUMBWA KWENYE SEKTA YA MICHEZO- WAZIRI MCHENGERWA


Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Mohammed Mchengerwa akizungumza katika kongamano la Michezo Wizara ikieleza mafanikio ya mwaka mmoja wa Serikali ya awamu ya Sita Madarakani. Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.Hassan Abbasi akiwasilisha mada katika kongamano la Michezo Wizara ikieleza mafanikio ya mwaka mmoja wa Serikali ya awamu ya Sita Madarakani. rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu kwa watu wenye Ulemavu (TAFF) Peter Sarungi akiwasilisha mada katika kongamano la Michezo Wizara ikieleza mafanikio ya mwaka mmoja wa Serikali ya awamu ya Sita Madarakani.

***********************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

WIZARA ya utamaduni, Sanaa na Michezo imeeleza mafanikio makubwa waliyoyapata katika kipindi cha mwaka mmoja wa Serikali ya awamu ya sita madarakani kwenye sekta ya Michezo.

Akielezea mafanikio hayo leo katika kongamano la Michezo Jijini Dar es salaam, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Mohammed Mchengerwa amesema katika kipindi hiki Ujenzi wa miundombinu mbalimbali ya Kisasa ya michezo kwa kukamilisha usanifu wa Uwanja wa Soka Dodoma unaotarajiwa kuchukua mashabiki takribani 100,000 na kuweza kuwa uwanja mkubwa ambao utakuwa ni kivutia nchini na hata barani Afrika.

Amesema katika kipindi hiki kumekuwa na ongezeko la bajeti ya Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo na Taasisi zilizo chini yake Hususani Baraza la Michezo Tanzania (BMT).

Aidha amesema kumekuwa na uanzishwaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Michezo sambamba na ubunifu wa chanzo madhubuti cha upatikanaji wa fedha kwa ajili ya mfuko huo kupitia mapato ya kodi ya Asilimia Tano (5%) yatokanayo na Michezo ya Kubashiri matokeo ya michezo (Sports Betting).

Hata hivyo amesema anatambua wapo baadhi ya viongozi ambao kwa kipindi kirefu wanaendesha shughuli za vyama kwa mazoea bila kufuata taratibu wala kuheshimu na kutii mamlaka zinazosimamia Michezo, na amefafanua kuwa katika kipindi chake masuala ya Rushwa, Ubadhirifu wa mali na fedha za Umma, Upendeleo na Unyanyasaji katika Michezo hatayavumilia.

Kwa upande wake rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu kwa watu wenye Ulemavu (TAFF) Peter Sarungi amefafanua kuwa kutokana na maono makubwa ya Mhe. Rais timu yao imefuzu kwenda kombe la dunia.

Amesema kutokana na utashi huo Mhe. Rais amefungua ajira kubwa za kitaifa na kimataifa kwa wachezaji walemavu ambapo hadi sasa wachezaji wanne (4) wameshapata timu katika mataifa mbalimbali Duniani.

Post a Comment

0 Comments