Ticker

6/recent/ticker-posts

SERIKALI KUONGEZA JUHUDI KUSHIRIKIANA NA WADAU KUREJESHA UOTO ILI KUEPUKANA NA MABADILIKO YA TABIA NCHI



************

NA Magrethy Katengu

Dar es salaam

Serikali imesema itajitahidi inaongeza jitihada za makusudi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kupanda miti ili kusaidia kuepukana athari ya mazingira inayosababishwa na shughuli za binadamu ikiwemo uchomaji mkaa utengenezaji mbao uchimbaji madini kwa kukataji miti ovyo inayopelekea uoto wa asili kupotea.

Akizungumza leo Mkuu wa wilaya ya Temeke Mhe Jakate Mwegelo Jijini Dar es salaam katika uzinduzi wa Mradi wa kupambana na mabadiliko ya tabia nchi utakaodumu takribani miaka kumi kwa utunzaji wa mazingira utakaohusisha upandaji miti na ukuzaji wa misitu unaosimamiwa na shirika lisilo la kiserikali (KIJANI PAMOJA) na Ubalozi wa Ireland nchini Tanzania ikiwa ni lengo la kurejesha uoto wa asili na kupambana na athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia Nchi

DC Joketi amesema ni budi kuweka jitihada kubwa kwa upandaji miti katika mikoa iliyoathirika zaidi kwa kupoteza uoto wa asili ikiwemo Dar es salaam kutokana na kuwa na viwanda kuwa vingi inayosababisha kuchafuka hali hewa ya inayoyola viwandano kutoruhusu uoto wa asili kuota kupotea kabisa baadhi ya maeneo hivyo amewaomba wadau kujitokeza kwa wingi kupanda uoto usio wa asili ili kupunguza madhara ya majanga yatokanayo na mabadiliko ya tabia Nchi

"Niseme kwamba kadri idadi ya watu inavyozidi kuongezeka ndivyo na uhitaji mkubwa wa maeneo kwa ajili ya kuishi na Shughuli za binadamu zinavyozidi kuathiri mazingira hivyo serikali peke yake kukabiliana na suala la utunzaji wa mazingira haliwezi unahitajika nguvu kutoka kwa wadau wengi "alisema DC Jokate.

Naye Katibu Mkuu dawa asilia na ulinzi wa mazingira Bonoventura Mwolongo amesema hitaji la upandaji miti ni muhimu kwani hutumika katika dawa chakula matunda kwa binadamu hutumika katika nyakati tofauti hivyo ni budi kuweka nguvu za ziada kurejesha kiasi Cha miti kilichopotea

"Ni hakika ymaisha yetu wanadamu tunategemea sana mimea ili kuishi kwa mahitaji yatu ya kila siku mimea hiyo tunatumia kwa chakula,matunda ,dawa,nishati hivyo ni budi tunavyotumia mimea hiyo kukumbukumbuka kanuni ya kata mti panda mti kwani tukiruhusu kuitumia mimea bila kuipanda mingine majanga yatokanayo na mabadiliko ya tabia nchi yatatuathiri wenyewe ikiwemo ukame,mafuriko"alisema Mwolongo

Naye Balozi msaidizi wa Ireland Nchini Tanzania ,Mags Gynor amesisitiza kupanda misitu ili kulinda Dunia dhidi ya majanga na ameasa Vita dhidi ya mabadiliko ya tabia Nchi ni suala la kidiplasia na kipaumbele Cha Maendeleo kwa Nchi yoyote hivyo wanayo furaha kuunga Mkono Tanzania kwa kuongeza juhudi katika kutunza mazingira ili kupambana na mabadiliko ya tabia nchi

Kwa upande wake Mbazi Malisa Mratibu Mradi KIJANI PAMOJA amesema katika Mradi huo utahisisha wadau mbalimbali ikiwemo wanafunzi,Wafanyabiashara,na watazunguka Nchi nzima kuhakikisha miti onapandwa na kutunza vizuri

Naye Mwanzilishi na afisa Mtendaji Mkuu Kijani Pamoja Sarah Scot amesema utunzaji wa uoto wa asili inafaida kubwa hususani kwa miji mikubwa na tafiti iliyofanywa Jijini Dar es salaam mwaka 2019 na shirika la ICLEI la nchini Ujermani kwa kushirikiana na Wizara ya ardhi nyumba na maendeleo ya Makazi ya watu imebainisha kuw jiji la Dar es salaam linapoteza uoto wake wa asili kwa kasi asilimia kumi misitu yake kwa mwaka na ifikapo 2040 litakumbwa na ongezeko la joto kufikia nyuzi 36'C kutokana na mabadiliko ya tabia nchi yanayosababishwa na uharibifu uoto wa asili na misitu

Post a Comment

0 Comments