*********************
MAKETE
Changamoto ya muda mrefu ya uhaba wa mashine za kuhifadhi watoto wanaozaliwa kabla ya wakati NJITI katika hospitali ya wilaya ya Makete mkoani Njombe Imepatiwa ufumbuzi na kurejesha matumaini ya kuishi kwa watoto na wazazi wanaokutwa na maswahibu hayo baada ya taasisi isiyo ya kiserikali kufika wiyani humo na kisha kubaini watoto njiti wapo kwenye hatari ya kupoteza maisha kwasababu ya kukosa huduma stahiki na kisha kuamua kutoa msaada wa mashine 3 za kufua oxgen zenye uwezo wa kunusuru maisha ya watoto 6 wanaozaliwa kabla ya muda.
Kwa mujibu wa ripoti ya mganga mkuu wa wilaya ya Makete imebainisha kuwa hospitali hiyo inamashine mbili tu za kuhifadhi watoto njiti ili hali kuna wakati wanapatikana watoto zaidi ya sita jambo ambalo huwalazimu kuwahamishia hospitali jirani hali inayohatarisha maisha ya watoto hao wawapo njiani.
Awali akikabidhi msaada wa mashine 3 za kufua oxgen kwa naibu waziri wa afya Dr Godwin Mollel zitakazotoa huduma kwa watoto 6 kwa wakati mmoja mkurugenzi wa taasisi isiyo ya kiserikali ya DORIS MOLLEL FOUNDATION amesema ameguswa na hali ngumu wanayopitia watoto njiti na wauguzi katika jitihada za kuokoa maisha yaO na kisha kuamua kutoa msaada huo wenye thamani ya shilingi mil 15 huku pia akigusia changamoto ya jengo la ICU kwa watoto wachanga hospitalini hapo.
Kwa upande wake mganga mkuu wa halmashauri ya wilaya ya Makete Dr Itikija Msuya anasema msaada huo umekuja wakati sahihi na unakwenda kuokoa masiha ya watoto waliyokuwa wakipoteza maisha kwasababu ya uchache mashine hizo huku baadhi ya wakazi wa Makete akiwemo Betrice Kyando akitoa hisia zake kwa msaada huo.
Mara baada ya kupokea msaada huo na kuikabidhi hospitali naibu waziri wa afya Dr Godwin Mollel akasema taasisi imeonyesha uzalendo mkubwa kushirikiana na serikali kudhibiti vifo vya mama na mtoto
Katika hatua nyingine waiziri Mollel ameweka bayana hatua zinazochukuliwa na serikali kuboresha sekta ya afya ikiwemo ujenzi wa kiwanda cha dawa za binadamu na mipira ya mkono mjini Makambako unaogharimu zaidi ya bil 19.
" Kwa miezi tisa tu tangu mama Samia aingie madarakani serikali imeanzisha miradi mikubwa mkoani Njombe ukiwemo wa kiwanda cha dawa za binadamu unaotekelezwa mjini Makambako,Alisema naibu waziri wa Afya Dr Godwin Mollel.
0 Comments