Ticker

6/recent/ticker-posts

TANGA UWASA YATUMIA BILIONI 22.2 UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAJI KATIKA KIPINDI CHA AWAMU YA SITA INAYOONGOZWA NA RAIS SAMIA

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly akizungumza na waandishi wa habari ambao hawapo pichani wakati akitoa taarifa ya miradi iliyotekelezwa katika kipindi cha Utawala wa Rais wa awamu ya Sita Samia Suluhu kwa mkoa wa Tanga
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly akizungumza na waandishi wa habari ambao hawapo pichani wakati akitoa taarifa ya miradi iliyotekelezwa katika kipindi cha Utawala wa Rais wa awamu ya Sita Samia Suluhu kwa mkoa wa Tanga ikiwa ni uzinduzi wa wiki ya Maji



Meneja wa Ufundi wa Tanga Uwasa Mhandis Rashid Shabani akizungumza na waaandishi wa habari leo wakati wa ziara yao ya kutembelea vyanzo vya maji eneo la Mabayani na Kituo cha Kutibu Maji cha Mabayani ikiwa ni ikiwa ni uzinduzi wa wiki ya Maji




Afisa Uhusiano wa Tanga Uwasa Devotha Mayalla akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo kushoto ni Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly

Afisa Uhusiano wa Tanga Uwasa Devotha Mayalla akizungumza na waandishi wa habari

Sehemu ya waandishi wa habari wakiwa eneo la bwala la Mabayani ambalo ndio chanzo cha Maji

Sehemu ya bwawa la Mabayani kama linavyoonekana



NA OSCAR ASSENGA,TANGA

MAMLAKA ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Tanga (Tanga Uwasa) kati ya mwezi Machi mwaka 2022 hadi sasa imetumia kiasi cha Bilioni 22,221,342,314 katika utekelezaji wa miradi 10 yenye lengo la kuboresha hali ya upatikanaji wa huduma za majisafi.

Sambamba na hilo pamoja na uondoshaji wa majitaka katika maeneo yake ya utoaji wa huduma Jijini Tanga na Miji ya Pangani na Muheza ambapo miradi hiyo inaendelea kutekelezwa na imefikia katika hatua mbalimbali za utekelezaji.

Hayo yalisemwa leo na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly wakati akitoa taarifa ya miradi iliyotekelezwa katika kipindi cha Utawala wa Rais wa awamu ya Sita Samia Suluhu kwa waandishi wa habari mkoani Tanga.

Aliitaja miradi hiyo kuwa ni uboreshaji wa hali ya upatikanaji wa maji Tanga awamu ya pili ambapo ujenzi wa mradi ulianza mwezi Agosti 2021 na unatarajiwa kukamilika Mwezi Agosti mwaka huu na unalenga kuboresha hali ya upatikanaji wa huduma ya maji kwa wakazi wa Jiji la Tanga na miji Jirani ya Kasera Mkinga na Muheza.

Alisema mradi huo utawezesha wakazi wa Tanga wapatao 382,092 kupata maji safi masaa 24 kwa siku kutoka wastani wa saa 21 kwa siku

Mhandisi Hilly alisema pia wanatekeleza mradi wa uboreshaji wa huduma ya maji safi Tanga kukabiliana na (Uviko 19) ambapo unatekelezwa kupitia fedha za miradi ya kuboresha tahadhari ya ugonjwa wa Uviko 19 ambapo unatekelezwa kwa lengo la kusogeza huduma ya maji kuwafikia wakazi wa maeneo tajwa wapatao 7200 ujenzi ulianza Desemba 2021 na utakamilika Aprili 2022.

Hata hivyo alieleza licha ya mradi huo wanatekeleza ujenzi wa miundombinu ya maji kuboresha upatikanaji wa maji Mitaa ya mpirani,ndaoya, Kibafuta, Mleni na Chongoleani ambapo mradi huo umeanza kutoa huduma katika vituo 19 vilivyounganishwa na mtandao wa maji.

“Miradi mingine ni ujenzi wa Bomba la Maji lenye kipenyo cha DN 300 wenye urefu wa mita 8200 kutoka Mowe hadi Pongwe na umekamilika mwezi Desemba 2021 na kwa sasa unatoa maji kwa wakazi wa Kata za Mlingano,Ngomeni,Lusanga,Mpapayu na Genge na wakazi wapatao 10,000 wamenufaika nao ”Alisema

Aidha Mkurugenzi huo aliutaja pia mradi wa ujenzi wa miundombinu ya Maji Safi Mji wa Muheza Mjini na ambapo mkandarasi wa ujenzi huo pamoja na mzabuni wa kuleta mabomba na viungio wameshapatikana na ujenzi wake utaanza mwezi machi 2022 na unatarajiwa kukamilika mwezi June mwaka huu huku wakazi 15,700 wakitarajiwa kunufaika.

“Mradi mwengine ni ujenzi wa miundombinu ya maji safi mji wa Pangani ambapo kwa sasa mkandarasi wa ujenzi pamoja na mzabuni wa kuleta mabomba na viunganishi wameshapatikana na ujenzi utaanza mwezi Machi mwaka 2022 na unatarajiwa kukamilika June 2022 na utaboresha upatikanaji wa maji kutoka masaa sita kwa siku kufikia masaa 12 kwa siku na kunufaisha wakazi wapatao 37,109”Alisema

“Pia kutakuwa na mradi wa ujenzi wa mabwawa ya ukusanyaji na kusafisha maji taka Muheza ambapo mji wa Muheza haukuwa na mfumo huo wa lakini mwaka huu fedha 2021/2022 Serikali imeweza kutekeleza ujenzi wa mfumo wa kukusanya,kutibu na kusafisha majitaka ikiwa ni pamoja na kununua gari la kukusanya majitaka toka kwa wakazi wa Muheza na maeneo Jirani”Alisema

Hata hivyo alisema pia utekeleza wa ujenzi wa mabwawa ya kukusanya na kusafisha maji taka Pangani ambapo mji huo haukuwa na na mfumo wa maji taka lakini mwaka huu wa fedha 2021/2022 Serikali imewezesha ujenzi wa mfumo wa kukusanya,kutibu na kusafisha majitaka ikiwa ni pamoja na kununua gari la kukusanya majitaka toka kwa wakazi wa Pangani ambao unawanufaisha wakazi wote wa Pangani na majirani wapatao 20,400 na mzabuni wa ujenzi ameshakabidhiwa eneo la ujenzi na mradi unatarajiwa kukamilika mwezi Agosti mwaka huu.

Akizungumzia miradi mengine alisema kuna miradi inayotekelezwa kwenye mji wa Tanga ambapo ni usanifu wa mradi wa miundombinu ya majitaka na usimamizi wa ujenzi ambao utakuwa na manufaa kutokana na miundombinu iliyopo ilijengwa miaka zaidi ya 60 iliyopita na hivyo imechakaa na mahitaji na gharama halisi za mradi na mhandisi shauri (WPCOS Co.Ltd )ameshaanza kazi ya usanifu Tanga Januaria 2022 na anatajiwa kumaliza mwezi June 2022.

Hata hivyo alisema pia wanaandaa taarifa ya udhibiti wa athari ya Mazingira na Jamii wakati wa utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa miundombinu ya majitaka ambapo manufaa yake ni kwamba mhandisi mshauri (Tansheq Co,Ltd) ameshaanza kazi ya kutafiti na hatimaye kuandaa taarifa ya athari katika jamii na mazingira na namna ya kudhibiti zile ambazo zitajitokeza wakati wa ujenzi wa mradi.

Post a Comment

0 Comments