Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Bw.David Ndibalema akizungumza katika hafla ya warsha ya sekta ya Umeme kuelekea maadhimisho ya siku ya Viwango barani Afrika 30,Machi 2022.Baadhi ya wadau mbalimbali wa Viwango wakiwa kwenye hafla ya warsha ya sekta ya Umeme kuelekea maadhimisho ya siku ya Viwango barani Afrika 30,Machi 2022
**************************
KATIKA kuelekea maadhimisho ya Siku ya Viwango Afrika Kitaifa kwa mwaka 2022, Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limeandaa shughuli mbalimbali ikiwemo warsha zitakazowahusisha wadau katika sekta ya utalii, umeme, madawa na vifaa tiba kwa lengo la kuwapa elimu juu ya viwango vya mifumo ya kimenejimenti kama ISO 9001, 14000 na nyinginezo ili kuwezesha taasisi zao kutoa huduma zinazokidhi viwango vya kimataifa.
Akizungumza katika hafla ya warsha ya sekta ya Umeme kuelekea maadhimisho ya siku ya Viwango barani Afrika 30,Machi 2022,Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Bw.David Ndibalema amesema viwango ni chombo cha kubadilishana maarifa, teknolojia na kanuni bora za utendaji katika shughuli za biashara, masuala ya kijamii na masuala ya kisheria.
Amesema awali TBS katika kusheherekea maadhimisho hayo liliratibu shindano la uandikaji wa insha kwa wanafunzi wa vyuo vikuu vyote nchini ambalo liliratibiwa katika ngazi ya Taifa ambapo mshindi atakayepatikana ataiwakilisha Tanzania katika mashindano ya ngazi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na baadae katika ngazi ya Afrika.
0 Comments