Ticker

6/recent/ticker-posts

TBS YAWATAKA WAZALISHAJI WA TOFALI KUFUATA MATAKWA YA VIWANGO

Mkuu wa Maabara ya Ujenzi TBS, Mhandisi Mahona William akitoa maelezo kuhusu umuhimu wa kufuata viwango katika uzalishaji wa tofali za saruji mara baada ya waandishi wa habari kufanya ziara ya kutembelea maabara za TBS leo tarehe 18/03/2022 Jijini Dar es Salaam

***********************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

WAZALISHAJI wa matofali ya saruji wametakiwa kuzalisha matofali ambayo yanakidhi viwango vya ubora ili kuepuka madhara makubwa yatakayojitokeza kwa mtumiaji.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Maabara ya Ujenzi TBS, Mhandisi Mahona William mara baada ya waandishi wa habari kufanya ziara katika maabara za Shirika la Viwango Tanzania leo tarehe 18/03/2022 Jijini Dar es Salaam.

Amesema tofali linatakiwa liwe limegandamizwa mchanga wa kutosha ambao utafanya tofali liwe imara na lenye kukidhi viwango vinavyotakiwa.

"Tunashauri kwa ujenzi wa kawaida angalau mfuko mmoja wa saruji uweze kutoa tofali 30 ambazo zitakuwa zinakidhi viwango vinavyotakiwa". Amesema

Waandishi wa habari wamefanya ziara hiyo kujifunza na kujionea mabara za TBS zinavyotekeleza majukumu yake katika kupima sampuli.

Post a Comment

0 Comments