Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe.Ng'wilabuzu Ndwata Ludigija akizindua wa huduma mpya ya Bima ya Hifadhi Biashara leo Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe.Ng'wilabuzu Ndwata Ludigija akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa wa huduma mpya ya Bima ya Hifadhi Biashara leo Jijini Dar es Salaam.
**************************
Wajasiriamli na Wafanyabiashara ndogo ndogo maarufu kama Machinga wametakiwa kujijengea mazoea ya kulinda biashara zao kwa kukata bima itakayolinda mitaji yao.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam wakati wa Uzinduzi wa huduma mpya ya Bima ya Hifadhi Biashara kutoka kampuni ya Howden Puri.
Akizungumza katika hafla hiyo Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe.Ng'wilabuzu Ndwata Ludigija amesema huduma ya Hifadhi Biashara itakuwa ni mkombozi kwa wafanyabiashara ndogondogo kutokana na wafanya biashara wengi wamekuwa wakipoteza mitaji yao kutokana na majanga ya ajali mbalimbali kitendo kinachorudisha nyuma uchumi wa kundi hilo kubwa hapa nchini.
Kwa upande wake Meneja Masoko kutoka kampuni ya Howden Puri Sinda Sinda akizungumzia huduma ya hifadhi Biashara amesema huduma hiyo ya Bima imeandaliwa kwa ajili ya kulinda mtaji wa wafanyabiashara ndogo ndogo na pindi inapotokea majanga mteja bima hiyo anasaidiwa kwa haraka ndani ya masaa 72.
Itakumbukwa kuwa serikali imekuwa na mpango wa kuhakikisha ifikapo mwaka 2030 kila mtanzania anakuwa na uelewa kuhusu Bima.
0 Comments