Ticker

6/recent/ticker-posts

WANANCHI WASHAURIWA KUTUMIA NISHATI MBADALA SERIKALI IKISHUGHULIKIA SUALA LA KUPANDA KWA BEI YA MAFUTA



*************

Na Magrethy Katengu

Wananchi wametakiwa kuwa wastahimilivu na bei za mafuta zilizopo kwani jitihada zinafanyika kuhakikisha Serikari inashusha tozo.

Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dar es salaam na Waziri wa Nishati Mhe.January Makamba wakati wa Uzinduzi wa Nembo Mpya ya Kampuni Total Engergies ambapo amesema serikali inaendelea kuhakikisha tozo zinapunguzwa ili kusaidia wananchi wasiendelee kuteseka.

Aidha Waziri Makamba amewashauri kutumia nishati mbadala ikiwemo gesi asilia kwani hali ya uuzwaji wa mafuta katika soko la Dunia ni kubwa na inaendelea kupanda siku hadi siku.

"Kupanda kwa bei haitalingana itategemeana maeneo na maeneo kutokana na usafiri hivyo hata bei za bidhaa zitapanda kidogo hivyo wananchi hawana budi kuwa wastahimilivu na bei kubadilikabadilika". Amesema Waziri Makamba.

Amesema Serikali itaendelea kuungana na Wadau mbalimbali wanaotoa huduma kwa wananchi ikiwemo Kampuni ya usambazaji wa mafuta ya Total Enrgies.

Sanjari na hayo Waziri Makamba ameipongeza Kampuni hiyo pia kwa kuzindua Kituo kipya cha Solar na kueleza kuwa hilo ni jambo kubwa na Maendeleo makubwa katika Sekta ya Nishati.

“Na sisi kama Serikali tunawaunga mkono kwa matumizi mazuri ya nishati jadidifu ikiwemo ya Jua. TotalEnergies ni Kampuni kubwa inayofanya kazi ya kuuza mafuta nchini kwa miaka 50 sasa, “ amesema Makamba.

Hata hivyo amesema wataendelea kuchukua hatua mbalimbali kuhakikisha wanapunguzia wananchi makali ya bei kupanda.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa TotalEnergies Jean Francois Schoepp ameihakikishia Tanzania kuwa Kampuni hiyo itaendelea kuzalisha bidhaa zenye ubora.

Naye Mwenyekiti wa Kampuni hiyo Aluko Olagoke amesema kuwa TotalEnergies imejidhatiti kuzalisha na kusambaza Nishati bora, safi ambayo itakuwa rahisi kwa kila mtu.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa kampuni ya TotalEnergies Jean Francois schoepp amesema lengo lakampuni hiyo ina vituo 100 Nchi nzima na mpaka sasa wameshafungua vituo 20 vinavyotumia nishati huku lengo lao ni kufungua vituo zaidi ya 60 vya nishati jua na bidhaa zake.

Post a Comment

0 Comments