Ticker

6/recent/ticker-posts

WAZIRI NDALICHAKO ATAKA MUONGOZO WA SADC WA KULINDA AJIRA KWA WATOTO KUZINGATIA MAADILI YA KIAFRIKA


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akichaangia jambo wakati wa Mkutano wa Mawaziri wa Kazi na Ajira kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) leo tarehe 30 Machi, 2022 Lilongwe, nchini Malawi.


Matukio mbalimbali katika Mkutano huo wa Mawaziri wa Kazi na Ajira kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) leo tarehe 30 Machi, 2022 Lilongwe, nchini Malawi yakiendelea.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) mara baada ya Mkutano wa Mawaziri wa Sekta ya Kazi na Ajira uliofanyika hii leo tarehe 30 Machi, 2022 Lilongwe, nchini Malawi.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Waziri wa Mambo ya Nje kutoka nchi ya Malawi, Mhe. Nancy Tembo.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi pamoja na Wataalamu alioambatana nao katika kikao hicho cha Mawaziri wa Kazi na Ajira kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) leo tarehe 30 Machi, 2022 Lilongwe, nchini Malawi.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (katikati) akisaini kitabu cha wageni alipotembelea Ubalozi wa Tanzania nchini Malawi. Kulia ni Balozi wa Tanzania nchini Malawi Mhe. Benedict Mashiba. Kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Chama cha Waajiri Tanzania, Bi. Suzanne Ndomba.

***************************

Na. Lusajo Mwakabuku, OWM-KVAU Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce L. Ndalichako amewataka wajumbe wa mkutano wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kuhakikisha katika mwongozo wa kulinda na kuzuia ajira mbaya kwa watoto ni vyema maneno yaliyotumika yakapatiwa tafsiri ili yaendane na maadili, utamaduni, na mazingira ya kiafrika.

Waziri Ndalichako alitoa kauli hiyo mapema leo 30/03/2022 jijini Lilongwe Malawi alipokuwa akishiriki Mkutano wa Mawaziri wa Kazi na Ajira wa SADC waliokutana kujadili mambo mbalimbali juu ya sekta ya Kazi na Ajira ambapo katika kikao hicho ajenda 13 zinazohusu kuweka miongozo mbalimbali ya kusimamia masuala ya ukuzaji wa fursa za ajira, usimamizi wa viwango vya kazi, hifadhi ya jamii na usalama na afya mahala pa kazi.

Akitoa mchango wake, Profesa Ndalichako alisema suala la biashara ya ngono kwa mila na desturi ya nchi zetu za Afrika ni suala lisilokubalika, hivyo alisisitiza katika mwongozo huo isitafsiriwe kuwa biashara hiyo inakubalika kwa wasio watoto peke yake kwani kwa mazingira na tamaduni zetu za kiafrika biashara hiyo ni haramu.

Masuala mengine yaliyojadiliwa katika kikao hicho ni pamoja na kupitia rasimu ya Itifaki ya SADC ya Kazi na Ajira, Mwongozo wa kuanzisha Taasisi za Majadiliano ya Waajiri na Waajiriwa, Zana za Ufuatiliaji na Utoaji taarifa kuhusu utekelezaji wa Mpango wa Uhamaji Nguvukazi ndani ya SADC pamoja na kuanzisha mfumo wa taarifa za soko la ajira wa SADC.

Pia mijadala mingine ilifanyika juu ya Hali ya Utekelezaji na Uridhiaji wa Itifaki na Mikataba ya Shirika la Kazi Duniani na pia mkutano huu ulipokea taarifa kuhusu maandalizi ya ushiriki wa nchi za SADC katika Mkutano Mkuu wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) unaotaratijwa kufanyika Mwezi Juni, 2022.

Post a Comment

0 Comments