Ticker

6/recent/ticker-posts

AMEND KUHAKIKISHA USALAMA BARABARANI KWA WATOTO KWENDA NA KURUDI SHULENI UNAIMARIKA.***********
Na Hamida Kamchalla, Tanga.

Takwimu zinaonesha kuwa, kila mwaka watu takribani Milioni 1.35 hupoteza maisha kutokana na ajali za barabarani huku wengine zaidi ya Milioni 50 wakijeruhiwa Duniani.

Hayo yamebainishwa na leo na Simon Kalolo ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi isiyo ya Kiserikali inayojihusisha na Usalama Barabarani nchini (AMEND), katika hafla fupi ya uzinduzi wa mradi wa barabara za vivuko kwa wanafunzi katika shule ya msingi Mwanzange, jijini Tanga.

Amesema kwa msaada wa BOTNAR FOUNDATION, wakishirikiana na wadau wengine wanatekeleza Mradi wa Usalama Barabarani kwa Shule za Msingi na Sekondani jijini Tanga ili kuhakikisha kwamba usalama wa watoto unaendelea kuwepo."Hili siyo suala dogo, ni tatizo la ambalo linaikabili dunia nzima, lakini cha kusikitisha zaidi ni kwamba, kwa siku moja tu, ni wastani wa watu wasiopungua 3,700 wanafariki dunia kutokana na ajali hizo" amebainisha Kalolo.

Aidha Kalolo amefafanua kwamba ajali hizo kidunia zinahusisha Bara la Afrika ambalo lina idadi kubwa ya ajali lakini lina magari machache ambayo hayazidi asilimia 2 ukilinganisha na Mabara mengine Duniani.

"Kitakwimu, kwa nchi za Afrika tuna magari asilimia 2 ukilinganisha na nchi nyingine Duniani kote, lakini tuna ajali zaidi ya asilimia 16, kwahiyo ni jambo la kutilia mkazo na ni lazima jitihada hizi ziwe za ushirikiano" amesema.

"Serikali ina jukumu kubwa kwa upande wa jeshi la polisi, kikosi cha usalama barabarani, lakini kuna wenzetu wa TARURA ambao wanashuhulika na miundombinu, kuna watu wa elimu, afya, lakini pia Mashirika binafsi na wananchi wote kwa ujumla kwasababu suala la usalama barabarani ni la kila mmoja wetu" amesisitiza.

Amesema kwa msaada wa BOTNAR FOUNDATION, wakishirikiana na wadau wengine wanatekeleza Mradi wa Usalama Barabarani kwa Shule za Msingi na Sekondani jijini Tanga ili kuhakikisha kwamba usalama wa watoto unaendelea kuwepo

Post a Comment

0 Comments