Ticker

6/recent/ticker-posts

KAMATI YA KUCHUNGUZA KUCHAFUKA KWA MTO MARA YAWASILISHA TAARIFA BUNGENI


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson akifungua kikao cha kuwasilisha taarifa ya Kamati ya Kitaifa ya Kuchunguza Chanzo cha Kuchafuka kwa Mto Mara kilichofanyika leo Machi 5, 2022 katika ukumbi wa Msekwa Bungeni jijini Dodoma. Kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji, Viwanda, Biashara na Mazingira Mhe. David Kihenzile.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akizungumza wakati wa kikao cha kuwasilisha taarifa ya Kamati ya Kitaifa ya Kuchunguza Chanzo cha Kuchafuka kwa Mto Mara kilichofanyika leo Machi 5, 2022 katika ukumbi wa Msekwa Bungeni jijini Dodoma.

Wabunge wakimsikiliza Mwenyekiti wa kuwasilisha taarifa ya Kamati ya Kitaifa ya Kuchunguza Chanzo cha Kuchafuka kwa Mto Mara Prof. Samwel Manyele wakati akiwasilisha taarifa ya kamati hiyo katika ukumbi wa Msekwa Bungeni jijini Dodoma leo Machi 5, 2022.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji, Viwanda, Biashara na Mazingira Mhe. David Kihenzile akifunga mafunzo kwa wabunge kuhusu uwasilishaji wa taarifa ya Kamati ya Kitaifa ya Kuchunguza Chanzo cha Kuchafuka kwa Mto Mara katika ukumbi wa Msekwa Bungeni jijini Dodoma leo Machi 5, 2022.

Wajumbe wa Kamati ya Kitaifa ya Kuchunguza Chanzo cha Kuchafuka kwa Mto Mara pamoja na wabunge wakiwa katika kikao cha kuwasilisha taarifa ya kamati hiyo katika ukumbi wa Msekwa Bungeni jijini Dodoma leo Machi 5, 2022.

(PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS)

Post a Comment

0 Comments