Ticker

6/recent/ticker-posts

MKE WA RAIS WA ZANZIBAR MAMA MARIAM MWINYI ATOA SADAKA YA FUTARI KWA WAZEE WA UZI LEO.

MKE wa Rais wa Zanzibar ambae ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Mama Mariam Mwinyi akisalimiana na Viongozi wa Mkoa wa Kusini Wilaya ya Kati Unguja baada ya kuwasili katika viwanja vya Skuli ya Msingi Uzi,kwa ajili ya kutoa Sadaka ya Futari kwa Wazee kuazia umri wa miaka 70 wa Shehia mbili za Uzi na Ngambwa na (kushoto kwake) Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe Rashid Hadidi.(Picha na Ikulu)

MKE wa Rais wa Zanzibar ambae ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Mama Mariam Mwinyi akimkabidhi mmoja wa Wazee wa Kijiji cha Uzi Sadaka ya Futari, aliyokabidhi kwa Wazee wa Shehia mbili za Uzi na Ngambwa , hafla hiyo iliyofanyika katika Skuli ya Msingi Uzi Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.(Picha na Ikulu)

MKE wa Rais wa Zanzibar ambae ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Mama Mariam Mwinyi akimkabidhi Misahafu Sheikh Ali Othman kwa ajili ya Madrasa na Misikiti ya Shehia ya Uzi na Ngambwa, hafla hiyo iliyofanyika katika Skuli ya Msingi Uzi.(Picha na Ikulu)

MKE wa Rais wa Zanzibar ambae ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Mama Mariam Mwinyi akizungumza na kutowa nasaha zake kwa Wananchi wa Uzi, wakati wa hafla ya kutoa Sadaka ya Futari kwa Wazee wa umri wa miaka 70, hafla hiyo iliyofanyika katika Skuli ya Msingi Uzi na (kushoto kwake) Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe.Rashid Hadidi.(Picha na Ikulu)

Post a Comment

0 Comments