Ticker

6/recent/ticker-posts

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA AZINDUA KINYWAJI CHA TANZANITE PREMIUM VODKA


*************************

Na Ferdinand Shayo ,Manyara.

Naibu Waziri wa Uwekezaji,Viwanda na Biashara Exaud Silaoneka amezindua Kinywaji kipya cha Tanzanite Premium Vodka kinachotengenezwa na kiwanda cha Pombe kali cha Mati Super Brands Limited kilichopo Mkoani Manyara pamoja na kuzindua jengo jipya la utawala la kiwanda hicho.

Exaud amepongeza juhudi za Mkurugenzi wa Kiwanda hicho David Mulokozi kwa uwekezaji aliofanya ambao umesaidia kutengeneza ajira nyingi pamoja kulipa kodi kwa serikali hivyo kuchangia maendeleo ya nchi.

Aidha amesema kuwa serikali itaendelea kuweka mazingira bora ya uwekezaji wa viwanda kwa wawekezaji wote ili waweze kuchangia maendeleo kupitia uwekezaji wao.

Mkurugenzi wa Kiwanda cha Mati Super Brands Limited David Mulokozi amesema kuwa kiwand hicho kimeweza kulipa kodi mbali mbali za serikali pamoja na kuajiri vijana wanaozunguka kiwanda hicho.

Mulokozi ameipongeza serikali ya awamu ya sita ya Raisi Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira bora ya uwekezaji nchini.

Mbunge wa Viti Maalumu Asia Halamga amempongeza juhudi za mwekezaji huyo kwa kuwa mstari wa mbele katika kuwekeza katika mkoa wa manyara na kuwataka Wawekezaji wengine waige mfano wake.

Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara mkoa wa manyara pamoja Musa Msuya amesema kuwa wataendelea kushirikiana na serikali katika kuhakikisha sekta binafsi inaendelea kuwa chachu ya maendeleo ya mkoa huo na taifa kwa ujumla.

Mkuu wa Wilaya ya Babati Lazaro Twange amesema kuwa tayari serikali imetoa fedha ya kujenga barabara ya lami kuelelea kwenye kiwanda hicho ili kurahisisha usafirishaji wa malighafi pamoja na bidhaa.

Post a Comment

0 Comments