Ticker

6/recent/ticker-posts

TABOA YAIOMBA LATRA KUFANYA MAREKEBISHO BAADHI YA SHERIA IKIWEMO ADHABU NA FAINI**************

Na Magrethy Katengu

Chama cha wamiliki wa Mabasi Nchini (TABOA) wameiomba Mamalaka udhibiti usafiri wa ardhini LATRA kufanya marekebisho ya Sheria mbalimbali ikiwemo sheria inayomtaka mmiliki wa Basi kupewa adhabu ya faini kutokana na kosa lililofanywa na dereva badala yake madereva waliofanya makosa ndio wapatiwe adhabu.

Pia, wameiomba Wizara husika kuruhusu Mabasi kusafirisha abiria kwa Masaa 24 kwani kumekuwa na uhitaji mkubwa kwa abiria kusafiri muda wa usiku kutokana na shughuli zao za kiuchumi

Hayo yamewasilishwa leo Jijini Dar es salaam na mjumbe wa Kamati mtendaji ya chama cha wamiliki wa mabasi Tanzania TABOA Elinas Emmanuel katika Mkutano uliowakutanisha Wamiliki wa mabasi Tanzania na wizara ya ujenzi na uchukuzi.

"Ukweli abiria wanaosafiri nyakati za usiku ni wengi ikilinganishwa na wanaosafiri asubuhi kwani madereva wanaofanya kazi asubuhi walio wengi hawana leseni wanakwepa sheria hivyo serikali iangalie hali ya barabara zilizopo kwa sasa usalama wake ukoje waruhusu mabasi kufanya kazi nyakati za usiku kwani vituo vya askari viko vingi barabarani iangaliwe namna bora"alisema Elinas.

Aidha, wamiliki hao wamelalamikia Mfumo wa ufuatiliaji mwenendo wa mabasi VTS kutokuwa rafiki na wenye kuleta hitilafu katika vyombo hivyo vya usafiri na kuwa mfumo huo bado haujafikia malengo yake ya kufungua mwendo wa magari hayo na kusababisha ajali.

Baada ya kusikiliza malalamiko na Mapendekezo ya wamiliki hao katibu mkuu wa wizara ya ujenzi na uchukuzi Gabriel Migire amesema wizara itaunda kamati maalum itakayochunguza mfumo wa VTS na kuleta mapendekezo ya maboresho ya mfumo huo ili kuondokana na malalamiko yanayotokana na mfumo huo kwenye vyombo vya safiri.

Hata hivyo, amesema LATRA Inaendelea na Mchakato wa Kuweka nauli kwa kwenye vyombo vya usafirishaji baada ya kutolewa mapendekezo kwa wamiliki wa vyombo hivyo kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta.

Post a Comment

0 Comments