Ticker

6/recent/ticker-posts

WATANZANIA WASHAURIWA KUPENDA BIDHAA ZINAZOZALISHWA NA WAZAWA NCHINI


Balozi wa Kampuni wa Herbel Product Bi.Shamsa Ford akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya kuwekeana saini ya mkataba.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Herber Product Hamza Rugwe akizungumza na Waandishi wa habari.

***************

Na Magrethy Katengu ----Dar es salaam

Licha ya kuwepo bidhaa nyingi zinazozalishwa nje na kuletwa ndani ya nchi Watanzania wameshauriwa kupenda bidhaa zinazozalishwa hapa Tanzania ili kusaidia bidha zinazozalishwa nchini nazo kupendwa na Nchi za nje ili kwani kutachochea uchumi wa kukua zaidi na zaidi.

Rai hiyo umetolewa leo Jijini Dar es salaam Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Buchi Herber product inayojihusisha na utengenezaji sabuni aina ya Tricona black seeds soap Hazim Rugwa wakati wa kuwekeana saini ya makubaliano ya mkataba na msanii wa bongo movie Shamsa Ford kuwa balozi wao kutangaza bidhaa hiyo inayosaidi kung'arisha ngozi kuiweka katika ubora,kuondoa harara na chunisi,kuondoa fangasi ambapo amesema bidhaa hiyo imetengenezwa kwa vitu vya asili.

Amesema bidhaa hiyo ya sabuni inalinda na kuboresha ngozi na inapambana na magonjwa mbalimbali ya ngozi.

"Tricona soap imetengenezwa na vitu vya asili ina vitamini A, B, C, D, E na vitamini ambavyo inalinda ngozi dhidi ya mipasuko,inaleta muonekano mzuri wa ngozi, inashambulia kila aina ya magonjwa ya ngozi na kutambulisha rangi halisi ya ngozi "amesema Dk Hazim.

Naye Balozi wa tricona soap Shamsa Ford ameishukuru watanzania wanaopenda bidhaa zinazozalishwa hapa Nchini kwani wanachochea vijana wengi kutotegemea kuajiriwa badala yake kuajiriwa hivyo yeye pamoja na kipaji alichonacho bado anafanya shughuli zake kuunga mkono azma ya serikali kufanya biashara na kulipa kodi hivyo hata kampuni hiyo wanalipwa Kodi
"Niwaase wananchi wenzangu Mimikabla ya kuingia mkataba wa kuitangaza bidhaa hii niliitumia kwanza takribani miezi miwili ili kujiridhisha na ubora wa bidhaa na ndiyo nikakubali kuingia nao mkataba wa kuitangaza "alisema Shamsa.

Aidha niwashauri wale wote wenye matatizo ya magonjwa ya ngozi Tricona soap ni mkombozi kwa ngozi za Watanzania wa jinsia zote matatizo ya ngozi yamekwisha watu waitumie itawaletea matokeo mazuri

Post a Comment

0 Comments