Ticker

6/recent/ticker-posts

WAZIRI GWAJIMA AWATAKA WANANCHI KUTOA USHIRIKIANO KUPINGANA NA UKATILI WA KIJINSIA

Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maaalum Dkt Dorothy Gwajima akiongea na wananchi wa kata ya Chamazi (hawapo pichani) , alipofanya ziara fupi kwenye kata hiyo leo Aprili 18,2022. Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maaalum Dkt Dorothy Gwajima akiongea na wananchi wa kata ya Chamazi, alipofanya ziara fupi kwenye kata hiyo leo Aprili 18,2022. Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maaalum Dkt Dorothy Gwajima akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kata ya Chamazi, alipofanya ziara fupi kwenye kata hiyo leo Aprili 18,2022. Mkurugenzi wa Halmashauri ya Temeke, Mhe.Elihuruma Mabelya akizungumza na wananchi mara baada ya Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maaalum Dkt Dorothy Gwajima kufanya ziara katika kata ya Chamazi Manispaa ya Temeke leo Jijini Dar es SalaamKamishna Msaidizi wa Huduma za Ustawi wa Jamii Tanzania,Bw.Baraka Makono akizungumza na wananchi wa kata ya Chamazi mara baada ya Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wanawake na Makundi Maaalum Dkt. Dorothy Gwajima leo Aprili 18,2022.Diwani wa Kata ya Chamazi jijini Dar es Salaam Lawrence Gama, akiongea wakati wa ziara ya Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maaalum Dkt. Dorothy Gwajima kwenye kata hiyo leo Aprili 18,2022. Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maaalum Dkt Dorothy Gwajima akipata picha ya pamoja na Kamati ya Ulinzi wa Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) mara baada ya Waziri huyo kufanya ziara katika kata ya Chamazi Jijini Dar es Salaam leo Aprili 18,2022. Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maaalum Dkt Dorothy Gwajima akipata picha ya pamoja na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Serikali mara baada ya kufanya ziara katika Kata ya Chamazi jijini Dar es Salaam leo Aprili 18,2022. Wananchi wa Kata ya Chamazi katika Manispaa ya Temeke, wakimsikiliza Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maaalum Dkt. Dorothy Gwajima alipofanya ziara katika kata hiyo leo Aprili 18,2022. Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maaalum Dkt Dorothy Gwajima akiongea na wananchi wa kata ya Chamazi mara baada ya kuwasili kwenye nyumba ambayo anahifadhiwa mwanafunzi ambaye alitakiwa aoelewe. kulia kwake ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Temeke, Mhe.Elihuruma Mabelya akiwa amembeba mtoto ambaye alikumbwa na unyanyasaji kwa kulawitiwa na baba yake mzazi.Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maaalum Dkt Dorothy Gwajima akiongea na wananchi wa kata ya Chamazi mara baada ya kuwasili kwenye nyumba ambayo anahifadhiwa mwanafunzi ambaye alitakiwa aoelewe mara baada ya kufanya ziara ya kutembelea kata hiyo leo Aprili 18,2022.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

****************

NA EMMANUEL MBATILO,DAR ES SALAAM

WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt.Dorothy Gwajima ameagiza kukamatwa kwa wale wote ambao wamehusika kumuozesha mwanafunzi wa kidato cha pili (15) shule ya Sekondari Chamazi iliyipo Jijini Dar es Salaam.

Waziri Gwajima ametoa tamko hilo leo mara baada ya kufanya ziara katika kata ya Chamazi na kutembelea eneo ambalo alipo binti huyo.

Amesema kitendo cha kumuozesha mwanafunzi ni kosa kisheria hivyo wale wote ambao wamehusika wanatakiwa kuchukuliwa hatua.

"Wale wote waliohusika, wazazi,washenga na mashuhuda walioshiriki kwenye shughuli ya kumuozesha binti huyu wote wamekiuka sheria ya mtoto na sheria ya elimu ambayo inamtaka mtoto apate nafasi ya kuendelea na masomo". Amesema Waziri Gwajima.

Aidha katika tukio hilo, Waziri alipokea taarifa ya kulawitiwa kwa mtoto mdogo (4) na baba yake mzazi ambaye kwasasa anashikiliwa na vyombo vya dora.

Pamoja na hayo Waziri Gwajima ameitaka jamii kuhakikisha inatoa ushirikiano wa kutosha pindi wanapoona na kusikia matukio ya unyanyasaji wa kijinsia yanatokea katika jamii.

Nae Mkurugenzi wa Halmashauri ya Temeke, Mhe.Elihuruma Mabelya amesema chanzo cha binti huyo kukubali kuolewa ni migogoro ndani ya familia yake.

"Migogoro ya kifamilia ilifanya aone yuko tayari kuolewa licha ya kuwa anasema moyoni hakuwa tayari kuolewa ila alitaka kuondokana na ugumu wa maisha na kigogoro hiyo. Niwaombe wWzazi familia zetu ziwe na umoja ili kuboresha ustawi wa maisha ya watoto wa kike," amesema Mabelya.

Pamoja na hayo Mhe.Mabelya amesema kama manispaa walijipanga vizuri kupitia kamati na hatimaye kuzuia ndoa hiyo ambayo ilikuwa ifungwe.

"Mimi kama mwenyekiti ya ulinzi wa mwanamke na mtoto siko nyuma katika kuhakikisha haki za wanawake na watoto zinalindwa ipasavyo, ustawi wa jamii ni pamoja na kuhakikisha haki zao zinalinswa ipasavyo,". Amesema

Kwa upande wake Ofisa Ustawi Manispaa ya Temeke, Bi.Lilian Mafole amesema Aprili 14, 2022 mchana walipigiwa simu na msamalia mwema kuwa mwanafunzi huyo anatarajiwa kufunga ndoa na Maulid Athuman Aprili 15, 2022 saa 2:00 usiku.

"Baada ya kupokea taarifa hiyo niliwasiljana na vitengo tofauti, tukafanya uchunguzi ili kufahamu vizuri mazingira ya tukio na tulifnjikiwa, siku ya tukio saa mbili usiku tulifika eneo la tukio tukiwa timu nzima ikiwemo mkuu wa shule na polisi,". Amesema B.Mafole.

Amesema mwanafunzi huyo alichukuliwa na kupelekwa katika nyumba maalumu sehemu ambako anaweza kupatiwa huduma za ushauri wa kisaikolojia na kuangalia namna ya kumrudisha shule.

"Baadaye tunatakiwa kufanya utaratibu asiweze kurudi tena katika shule aliyokuwa anasoma kwa ajili ya maendeleo yake,". Ameeleza.

Post a Comment

0 Comments