Ticker

6/recent/ticker-posts

WAZIRI JAFO AWASILISHA BAJETI YA MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA MPANGO NA BAJETI KWA MWAKA 2021/22


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiwasilisha Bungeni Mapitio ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa mwaka 2021/22 na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2022/23 leo Aprili 27, 2022.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiteta jambo na Naibu Waziri wake Mhe. Khamis Hamza Khamis wakati wa uwasilishaji wa Mapitio ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa mwaka 2021/22 na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2022/23 leo Aprili 27, 2022.


Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Maganga (kushoto mbele) akiwa na Menejimenti ya Ofisi hiyo pamoja na Menejimenti ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) wakifuatilia hotuba ya Mapitio ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa mwaka 2021/22 na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2022/23 leo Aprili 27, 2022.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiteta jambo na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Maganga mara baada ya kupitishwa kwa hotuba ya Mapitio ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa mwaka 2021/22 na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2022/23 leo Aprili 27, 2022. Wengine kushoto ni Naibu Katibu Mkuu (Muungano) Bw. Abdallah Hassan Mitawi na Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Bw. Edward Nyamanga.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya Ofisi hiyo, wataalamu pamoja na Menejimenti ya Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) mara baada ya kupitishwa kwa hotuba ya Mapitio ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa mwaka 2021/22 na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2022/23 leo Aprili 27, 2022.

******************************

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo amewasilisha Bungeni Mapitio ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa mwaka 2021/22 na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2022/23.

Akiwasilisha hotuba hiyo leo Aprili 27, 2022, Dkt. Jafo amesema Ofisi ya Makamu wa Rais itaendelea kuratibu utatuzi wa changamoto za Muungano zilizobakia na zitakazojitokeza katika utekelezaji wa masuala ya Muungano kupitia Vikao vya Kamati ya Pamoja ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SJMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) ya Kushughulikia Masuala ya Muungano.

Aidha, Waziri Jafo alisema Ofisi itaendelea kuratibu Masuala ya Kiuchumi na Kijamii; Kuratibu masuala yasiyo ya Muungano kupitia vikao vya ushirikiano vya Wizara, Idara na Taasisi za SJMT na SMZ zisizo za Muungano zenye majukumu yanayoshabihiana; kutoa elimu kwa Umma kuhusu Muungano na kuratibu utekelezaji wa masuala 22 ya Muungano.

Aliongeza kuwa katika kuhakikisha hifadhi endelevu ya mazingira, kwa mwaka 2022/23, Ofisi imepanga kutekeleza vipaumbele sita ambavyo ni kuratibu utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Mazingira ya Mwaka 2021; kuratibu utekelezaji wa Mpango Kabambe wa hifadhi ya Mazingira na kufanya mapitio ya Sheria ya Usimamizi wa Mazingira, Sura 191.

Vipaumbele vingine ni kuratibu utekelezaji wa Kampeni Kabambe ya Hifadhi na Usafi wa Mazingira; kuendelea kujenga uwezo kwa jamii katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya Tabianchi na kuendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira.

Baada ya michango mbalimbali ya wabunge Bunge limeidhinisha makadirio ya jumla ya Sh. 53,116,317,000 kwa mwaka wa fedha wa 2022/23.


Post a Comment

0 Comments