Ticker

6/recent/ticker-posts

WAZIRI NAPE NNAUYE ATOA MAAGIZO KWA MKUU WA MKOA TANGA.

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Tekinolojia ya Habari Nape Nnauye kushoto, Meya wa jiji la Tanga Abdulrahman Shillow wa pili kushoto mwenye kanzu na mkuu wa Mkoa wa Tanga Adam Malima katikati wakiongea Jambo nje ya nyumba mojawapo waliyoweka anuani ya makazi jijini Tanga.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye akiangalia ramani ya mitaa iliyokuwa na namba za kuweka anuani za makazi kabla ya kuzindua zoezi hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Adam Malima akimpokea Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Tanga.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Adam Malima akiwa meza kuu na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye wakifuatilia wajumbe wa kikao..

*************

Na Hamida Kamchalla, TANGA.


WAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amemuagiza mkuu wa Mkoa wa Tanga Adam Malima kushuhulika na watendaji wanaokwamisha oparesheni ya kufuatilial utekelezaji wa anuani za makazi mkoani humo.

Nnauye ameyasema hayo alipokuwa katika ziara fupi ya utuatiliaji pamoja na kuzindua mradi huo huku akieleza kwamba Mkoa huo umefanya vibaya na kushika nafasi ya pili kutoka mwisho hivyo kiongozi yeyote aliyeshiriki kukwamisha zoezi hilo hatovumiliwa.

Amebainisha kwamba lengo la ziara hiyo ni kuja kuongeza nguvu kwenye operesheni ambayo Rais ameianzisha lakini pia kuhakikisha kwamba pale walipokwama wakwamue, na kwamba baadhi ya wataalamu wamefafanua kwamba upo mfumo ambao unafuatilia matumizi kila siku na wanaona mambo yanavyoenda.

"Na tangazo la operation ya Rais haijawahi kushindwa, tarehe iliyotangazwa ni lazima itakuwa hata kama tutahamia Tanga, kwa sababu lazima iwe, na wale wanaotukwamisha bahati mbaya inabidi watupishe, kwa sababu hii haina kushindwa" amesema

"Mkuu wa mkoa mimi nakuamini sana, wewe siyo mtu wa kushindwa, sababu ya kushindwa wewe huna na nia ya kushindwa huna, kwahiyo, nakushauri shuhulika na wale wanaokukwamisha, kama kuna shida katika utekelezaji wa jambo hili tuone namna ya kulitatua" amesisitiza.

Aidha Nnauye amesema kuwepo kwenye Mkoa ambao kuna halmashauri imefika asilimia 90 na kuna halmashauri nyingine kuna asilimia 0, ni dhahiri kwamba mwenye sifuri hatakuwa na jambo zuri la kumwambia na kumpendeza Rais.

"Mimi nataka kuwaambieni kwamba hakuna kushindwa kwenye jambo hili, na sisi kama Wizara tumesema na Katibu mkuu tukaongeza nguvu, tukaleta wataalamu tukwamue, kwasababu tunataka wote twende pamoja, hatuna nia ya mtu kuadhibiwa kwasababu ya kushindwa, labda ifike mahali ushindi kane kabisa kwamba huwezekani hapo tutakuwa hatuna namna" amesisitiza.

Hata hivyo amebainisha kwambaa ni vizuri viongozi wa maeneo husika waone aibu, kama wenzao wanaweza kwenda asilimia 90 na wewe ukawa na asilimia 0 na hii ili kufanikiwa ushirikiano mkubwa wa viongozi Taasisi mbalimbali unahitajika.

"Tumekuja kukumbusha kwamba hii ni oparesheni iliyotangazwa na Rais, siyo zoezi la kawaida, kwahiyo msilichukulie kikawaida, maana yake kuliangusha jambo hili ni kumuangusha Rais, jambo ambalo halikubaliki na mimi nataka kuwa muungwana kabisa" ameeleza.

"Sasa tisifike huko ambako itabidi tukaziane uso, hili jambo siyo la mkuu wa Mkoa peke yake bali ni la viongozi wote na nimesema kusudi Tanga mmefanya vibaya ili waamke wafanye vizuri ni aibu kwakuwa ninyi mlianza kuweka anuani za makazi kabla ya sehemu zingine, sasa msiniangushe Tanga" amesema Waziri Nape.

Naye mkuu wa Mkoa wa Tanga Adam Malima amekiri kuwepo kwa tatizo hilo na kumuahidi Waziri kwamba atalifanyia kazi na kulifanikisha kwa wakati kwa kushirikiana na wataalamu wa Mkoa huo.

"Mpaka kufikia leo tumeweza kutekeleza kwa asilimia 32, kwahiyo nikuhakikishie mpaka kufikia Aprili 30 mwaka huu nitakuwa nimekamilisha kwa asilimia 70 na nakuahidi Tanga itaendelea kufanya vizuri, na yeyote atakayethubutu kutukwamisha nitahakikisha anakaa pembeni" amesema

Post a Comment

0 Comments