Ticker

6/recent/ticker-posts

ZIFF KUMEKUCHA TAMASHA LA FILAMU KWA KISHINDO CHA SHAMRASHAMRA NDEREMO NA VIFIJO


Mratibu muandaaji wa ZIFF filamu Prof. Martini Muhando akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa taarufa kuhusu ujio wa Tamasha la ZIFF,kulia kwake ni Balozi wa Ulaya nchini Tanzania Manfredo Fauti.

***********
Na Magrethy Katengu

Ikiwa imesalia siku kadhaa kuelelea katika Tamasha la ZIFF, wasanii waigizaji nchi wameshauriwa kuendelea kufanya kazi zao vizuri ili ziendane na viwango vya kimataifa na kushindanishwa katika mashindano mbalimbali ili kusaidia wasiachwe na fursa zitakazojitokeza kwani matamasha hayo yamekuwa na faida kubwa kwao kujiongezea ujuzi na kujitangaza.

Rai hiyo imetolewa na Mratibu wa Tamasha la kimataifa la filamu Zanzibar(ZIFF) Prof. Martini Muhando ambapo amesema Mwaka huu wanaanzisha jukwaa la kudumu la ZIFF kwenye YouTube kwa filamu zilizopata kuoneshwa katika tamasha hilo yaani ZIFF@25 Retrospective.

Mrejeo huo utajumuisha filamu ambazo zimeshinda au kuvutia katika ZIFF hivyo tumekusudia jukwaa letu la Youtube liwe kituo cha kuangalia nmajadiliano ya ambapo watengenezaji filamu wataweza kufikia hadhira muhimu na kufanya mazungumzo nao.

"Tunazungumzia fahari waliyonayo Watanzania kwa ujumla katika ZIFF, kwa kuwa miongoni mwa matamasha matatu bora ya filamu barani. ZIFF sio tu imedumu pale ambapo wengine wameshindwa bali pia imejitengenezea misingi imara wa kuendelea. Udhaifu wowote ambao ZIFF inaweza kuonyesha, tutabaki kujivunia hivyo, ndio maana tunasema Lake Mtu Halimtapishi!"alisema Prof Muhando.

Sanjari na hayo kama kawaida, tamasha litawasilisha programu zake ikiwa ni pamoja na Panorama za Wanawake, Watoto na Vijiji ambapo tunaangazia filamu na shughuli zinazozunguka vikundi vitatu vya jamii.

Kwa kuungwa mkono na Umoja wa Ulaya (EU), mwaka huu, tutafanya shughuli za filamu na utamaduni Pemba baada ya kushindwa kufanya hivyo mwaka jana. Kutakuwa na maonyesho ya filamu juu ya mada ya wanawake na ujasiriamali, na vikundi vya uzalishaji vya wanawake vitafadhiliwa kuzalisha sanaa za mwonekano wa ZIFF na bidhaa nyinginezo.

"Mwaka huu tamasha hili pia litajumuisha warsha kuu 6 zitakazotolewa na wakufunzi wanaotambulika zikiangazia jukumu la tamasha kwa taaluma ya filamu barani Afrika. Warsha hizo ni pamoja na- On Documentary (Docubox- Kenya); uandishi wa vipindi vya TV (Pilipili Entertainment, Tanzania); Wanawake na Filamu (EU); Maabara ya filamu fupi (Kenya/Wales); Utengenezaji filamu wa majaribio (Hispania na Ajabu-Ajabu); Uhariri wa filamu (Off-courts-Ufaransa)"alisema Prof Muhando

Pia Warsha za Wanawake na Filamu itawasilisha maoni ya waongozaji wa filamu wanawake jinsi wanavyoendeleza wahusika wao wanawake, na vile vile wanavyotamani watazamaji wawatambue. Kwa hivyo tunawaalika watengenezaji filamu wanawake kufichua jinsi wanavyofanya kazi.

Darasa la Master juu ya vipaji vipya vya Sinema na Chipukizi (pamoja na maonyesho), litaendeshwa na Luis Patino, talanta inayochipukia ya Uhispania katika uongozaji wa filamu huku waigizaji wake pamoja na wahudumu wake wakija mwezi wa Mei kutayarisha filamu Zanzibar, kutakuwa na fursa kwa wataalamu na wanovice kushiriki na kujifunza mbinu mpya katika ubunifu na utayarishaji wa filamu.

Hata hivyo Mipango kadhaa ya kikanda ya filamu itazinduliwa wakati wa ZIFF ikiwa ni pamoja na kikao cha kwanza cha The East Africa Screen Collective (EASC), ambao ni muungano wa makampuni na mashirika yanayotetea uhuru wa simulizi katika sekta ya sanaa katika Afrika Mashariki.

Deutsche Well Akademie (DWA) itakusanya vikundi vya kwanza vya watu binafsi wanaofadhiliwa katika maendeleo ya filamu kutoka Ethiopia, Uganda na Tanzania.

Madhumuni ni kukutana, kusalimiana na kubadilishana uzoefu kuhusu maendeleo ya filamu. DWA ndio wenyeji wa hafla hiyo kwa kushirikiana na Film Lab Zanzibar ili kujenga vipaji kupitia mfuko huo nchini Tanzania.

Programu za nchi za Afrika, Karibea na Pasifiki (ACP) zitazinduliwa katika ZIFF2022 zikizileta pamoja nchi za ACP katika utayarishaji-shirikishi na mafunzo ya filamu, na Docubox itakuwa mwenyeji.

Naye Balozi wa Ulaya Nchi Tanzania Manfredo Faut amesema Utamaduni na Sanaa ni kitu Cha muhimu kinatangaza Taifa na kinatengeneza fursa mbalimbali za ajira kiuchumi hivyo vijana wasibweteke wajitokeze kukuza vipaji vya walivyo navyo

Aidha watu wote wadau wanakaribishwa kushiriki katika tamasha na kusapoti tamasha hilo linalotarajiwa kufanyika julai mwaka huu

Post a Comment

0 Comments