Ticker

6/recent/ticker-posts

COSTECH YASISITIZA BUNIFU ZENYE TIJA



***************

Serikali kupitia Tume ya Taifa ya sayansi na telnolojia-COSTECH imesema inatazamia kuweka kumbi za bunifu nchi nzima ili serikali iweze kuzalisha vijana wengi wanaofanya kazi za kibunifu zilizolenga kutatua changamoto ndani ya jamii.

Akizungumza wakati wa kufunga wiki ya ubunifu Kwa mkoa wa dar es salaam ambayo ilikuwa inafanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Mkurugenzi wa COSTECH, Dokta Amos Nungu amesema Tume itahakikisha ubunifu unakuwa agenda ya kudumu na pia inapata mrejesho kutoka Kwa wadau mbalimbali wa ubunifu waliohudhuria wiki hiyo ili nchi iwezekuwa na bunifu zenye tija.

“Kupitia Wiki ya Ubinifu ambayo imefanyika kwa siku tatu hapa Dar es Salaam tunachofurahi ni kuona ushiriki mkubwa wa wadau sambamba na kupokea maoni na mawazo yenye lengo la kuboresha bunifu zinazobuniwa na Watanzaniana.Kupitia maoni ya wadau tutajua tuboreshe wapi," Amesema Mkurugenzi Nungu.

Aidha amesema kuwa Wiki ya Ubunifu kitaifa ndio mara ya kwanza kufanyika kufuatia agizo la Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa mwaka Jana katika wiki ya Ubunifu alipoagiza maadhimisho yafanyike nchi nzima, ambapo kwa mwakaa huu tume imeanza na mikoa 15.

Amesema wiki ya ubunifu ni jukwaa linalotoa mrejesho Kwa serikali kuona wapi iboreshe na pia inasaidia wabunifu kuonesha bunifu zao nakutoa maonin Yao kwenye midahalo ambayo serikali inayapokea na kuyafanyia kazi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa digitali na Huduma za ziada kutoka VODACOM, Nguvu Kamando amesema kuwa Vodacom wapo mstari wa mbele katika kuhakikisha teknolojia inaendelea kutumimika nchini na watanzania wengi.

Wiki ya Ubunifu Tanzania imeratibiwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kushirikiana na COSTECH pamoja na UNDP kupitia program ya Funguo na mdhamini mkuu wa wiki hiyo ni Kampuni ya Simu ya Vodacom.

Post a Comment

0 Comments