Ticker

6/recent/ticker-posts

JESHI LA POLISI IRINGA LINAMSHIKIRIA CHENGULA KWA TUHUMA ZA KUMSHAMBULIA NA KUMJERUHI MKAZI WA MANISPAA YA IRINGA KWA KUTUMIA KITAKO CHA BASTOLA

Kamanda wa polisi mkoani Iringa ACP Allan Bukumbi akionyesha baadhi ya vitu ambavyo vimekamtwa kwenye uhalifu uliofanyika katika baadhi ya wananchi wa mkoa wa Iringa

Kamanda wa polisi mkoani Iringa ACP Allan Bukumbi akionyesha baadhi ya vitu ambavyo vimekamtwa kwenye uhalifu uliofanyika katika baadhi ya wananchi wa mkoa wa Iringa na hilo gari lilitumika katika kufanya shughuli za utapeli kwa wananchi wa Iringa


Na Fredy Mgunda,Iringa.

MMILIKI wa shule ya Sun Academy mkoani Iringa Nguvu Chengula anashikiria na Jeshi la Polisi mkoani humo kwa tuhuma za kumshambulia na kumjeruhi kwa kutumia Kitako cha bastola mkazi wa manispaa ya Iringa Alifa Mkwawa baada ya kuibuka mzozo wa mtuhumiwa kugoma kutoa ushamisho wa mtoto wa mjeruhiwa.

Kwa mujibu wa Kamanda wa polisi mkoani Iringa ACP Allan Bukumbi akitoa taarifa ya matukio ya uhalifu kwa waandishi wa habari mkoani humo alisema tukio hilo limetokea mnamo Mei 16 mwaka huu majira ya saa sita mchana ambapo inadaiwa kuwa mjeruhiwa Alifa Mkwawa alifika katika ofisi ya Shule ya Sun Academy kwa lengo la kufuatilia uhamisho wa Mtoto wake aliyefahamika kwa jina la Leonard Wilbert Mkwawa (6) anayesoma darasa pili shuleni hapo ambapo Mtuhumiwa aligoma kutoa uhamisho huo hali iliyozusha majibizano yaliyopelekea mtuhumiwa kutoa bastola na kufanya shambulizi hilo

ACP Bukumbi alisema kuwa licha ya mtuhumiwa kumiliki bastola hiyo kihalali aina ya Canik 55 yenye namba 6472-15100082, lakini ameitumia isivyo halali hivyo Jeshi la Polisi linaendelea kushikilia Mtuhumiwa huyo Nguvu Chengula akiwa na kielelezo cha bastola hiyo wakati likiendelea na upelelezi kabla ya kumfikisha mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.

Alisema kuwa katika kupambana na kutokomeza matumizi na biashara haramu ya dawa za kulevya jeshi la polisi mkoa wa Iringa kwa nyakati tofauti maeneo ya vijiji vya Irambo na Ibumu kata ya Image wilaya ya Kilolo jeshi la polisi lilifanikiwa kumkama watuhumiwa watano na kuharibu mashamba ya matu ya bangi iliyolimwa kwa mchanganyiko wa mahindi na maharage.

ACP Bukumbi alisema kuwa watumiwa walitumia mbinu ya kulima vishamba vidogo mtawanyiko na kupanda bangi katika ya mazao hayo kwenye maeneo ya misitu na makorongo ambapo mashamba hayo yanamilikiwa na Benjamin Mkapa Ngulo na shamba linguine linamilikiwa na Teso Wilbath ambao kwa ujumla mashamba yote yanaukubwa wa ekari mbili na nusu.

Alisema kuwa watumiwa wanane walikamatwa kwa kujihusisha na kilimo cha bangi na mtuhumiwa mmoja amekamatwa kwa kosa la kupatikana na bangi kilolo mbili.

Katika hatua nyingine Kamanda wa polisi mkoani Iringa ACP Allan Bukumbi alisema kuwa jeshi hilo linamshikiria mwanamke mmoja anaitwa Desderia Mbwelwe mwenye umri wa miaka 56 kwa tuhuma za kumlazimisha kufanya mapenzi na mtoto mwenye umri wa miaka nane (8) ambaye ni mwanafunzi wa darasa la tatu katika shule ya msingi Lumuli.

ACP Bukumbi alisema kuwa mwanamke huyo alifanikiwa kukamata mwanafunzi huyo kasha kumvutia kichakani na kumalzimisha kufanya mapenzi kwa kutumia nguvu kitendo kilichopelekea maumivu makali sehemu za siri za mtoto huyo na jeshi la polisi mkoa wa Iringa linamshikilia mtuhumiwa huyo na upelelezi ukikamilika litamfikisha mahakamani.

Alimaliaz kwa kuesma kuwa jeshi la polisi mkoa wa Iringa linawashikilia watu watatu wakiwa na mabunda ya karatasi nyeusi zilizokatwa na kupangwa mfano wa pesa za kitanzaia ambao walikuwa wamepanga kufanya utapeli mkoani humo wakitumia gari aina ya Mark x yenye rangi nyeupe namba za usajili ni T979 DWN inayomilikiwa na Herieth Khamis Mkazi wa Dar es salaam.

Alisema kuwa baada ya upekuzi waliwakuta na vipeperushi vya Sharif Majini,Pete za Bahati,Dawa aina ya IODINE,Vitamini B complex ambayo imechanganywa na maji na mara baada ya kufanya nao mahojiano walikiri kufika mkoa wa Iringa kwa lengo la kufanya Utapeli jambo ambalo halikufakiwa baada ya jeshi la polisi kuwakamata.

Post a Comment

0 Comments