Ticker

6/recent/ticker-posts

MWAKILISHI MKAZI WA AfDB AWASILISHA BARUA ZA UTAMBULISHO

Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) nchini Tanzania, Bibi. Patricia Laverley amewasilisha Barua za Utambulisho kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Libarata Mulamula katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Baada ya kupokea barua za utambulisho, viongozi hao pamoja na mambo mengine, walijadiliana masuala ya miundombinu endelevu pamoja na uboreshaji wa mazingira katika sekta binafsi.

Bibi. Laverley amemhakikishia Balozi Mulamula ushirikiano wa kutosha kutoka AfDB katika kuchochea utekelezaji wa miradi mbalimbali inayofadhiliwa na bank hiyo hapa nchini.

Nae Balozi Mulamula amemhakikishia ushirikiano wa kutosha kutoka Serikalini wakati wote wa utekelezaji wa majukumu yake hapa nchini na kuonmgeza kuwa AfDB imekuwa mdau mkubwa wa maendeleo ya Tanzania jambo ambalo ni ishara ya uhusiano mzuri uliopo baina ya Tanzania na bank hiyo.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Libarata Mulamula akipokea barua ya utambulisho kutoka kwa Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) nchini Tanzania, Bibi. Patricia Laverley katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Libarata Mulamula akizungumza na Mwakilishi Mkazi wa AfDB nchini Tanzania, Bibi. Patricia Laverley katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Mazungumzo ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Libarata Mulamula na Mwakilishi Mkazi wa AfDB nchini Tanzania, Bibi. Patricia Laverley yakiendelea katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Libarata Mulamula akiagana na Mwakilishi Mkazi wa AfDB nchini Tanzania, Bibi. Patricia Laverley yakiendelea katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam


Post a Comment

0 Comments