Ticker

6/recent/ticker-posts

RC MAKALLA ATANGAZA RASMI MSAKO MKALI KUKABILIANA NA PANYAROAD


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe.Amos Makalla akizungumza katika kikao kazi Cha kamati ya Ulinzi na usalama katika mkoa huo.
Wanakamati wa kamati ya ulinzi na usalama Mkoa wa Dar es salaam wakiwa katika Mkutano na Mkuu wa Mkoa Mhe.Amos Makalla leo Jijini Dar es Salaam.

***********

Na Magrethy Katengu

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla ameagiza kamati ya Ulinzi na Usalama kufanya oparesheni kabambe kuanzia usiku wa leo kuwasaka vijana maarufu kama Panyaroad wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu kwa kujeruhi watu nakupora vitu mbalimbali ikiwemo fedha,simu,na tiv

Agizo hilo amelitoa Jijini Dar es salaam katika kikao kazi na kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa huo lengo ni kujadiliana mikakati ya kuweza kupambana na uhalifu wa vijana wanaotembea mitaani na silaha mbalimbali ikiwemo mapanga nakupora mali mbalimbali ikiwemo Tv ,Simu na fedha na kwenda kuuza

"Naisisitiza kamati ya ulinzi na Usalama Mkoa wa Dar es salaam kuhakikisha inatoa taarifa kila siku kwa kuwapiga picha Kisha kuwasambaza mitandaoni ili kusaidia katika oparesheni ya kupambana na vikundi hivyo vya uhalifu(Panyaroad) ili kusaidia wazazi wa watoto hao kufahamu watoto wao walipo"alisema RC Makalla

Hata hivyo amewataka Wakuu wa Wilaya ,wakuu wa vituo vya polisi wilaya, kufanya msako kila mahali ili kuwabaini na kuwakamata wafanya biashara wote wanaonunua bidhaa za wizi kutoka kwa wahalifu hao ili kusaidia kutokomeza uhalifu wa panyarod wanaosumbua wananchi Jijini Dar es salaam.

Pia amesema vikundi hivyo ni vya watu wachache wanaotumia silaha zisizo na viwango ambapo wamefanya tukio kunduchi na katika nyumba 23 na kujeruhi watu 19 bila huruma hivyo ni Jambo la kusikitisha katika operesheni hiyo ihakikishwe wanabanwa kuwataja na wenzao waliojificha

"Kila siku tutoe taarifa ya mafanikio ya oparesheni hii ,pia panyaroad mnapowakamata wapigeni picha nakuwaweka mitandaoni ili wajulikane,hii oparesheni ninayoizindua leo isiwe ya kimyakimya ,Mambo matano niliyoyaelekeza yawe yakudumu kukabiliana na panyaroadi " amesem RC Makalla.

Naye Kamanda wa Jeshi la polisi Kanda Maalumu Dar es salaam ACP Jumanne Muliro amesema mwezi Aprili Mwaka huu Jeshi hilo limeendesha opereshe nakufanikiwa kuwakamata vijana wapatao 15 wenye umri kuanzia miaka 13 na kuendelea wanaosadikiwa ni panyaroad nakwamba wanaendelea kushikiliwa kwamahojiano zaidi na wametoa ushirikiano kuwataja wenzao

"Vijana wanaondelea na uhalifu mwisho wao umefika ,wazazi wao wawaonye watoto wao kwani kwa Sasa wakikamatwa watapigwa picha na kusambazwa katika mitandao ya kijamii ili wajulikane na ndugu zao wapate taarifa za haraka mahali walipo"amesisitiza Acp Muliro.

Vikundi vya Vijana maarufu Kama Panyaroad vimeanza kuibuka tena hivi karibuni huko Chanika Wilaya ya Temeke,Tabata wilayani Ilala na Kunduchi wilaya ya Kinondoni na kuanza kufanya vitendo vya kiuharifu ikiwemo kuvamia na kukata mapanga nakujeruhi wananchi huku wakipora vitu mbalimbali.

Post a Comment

0 Comments