Ticker

6/recent/ticker-posts

SERIKALI YATOA MSAMAHA WA RIBA KWA WAAJIRI WALIOCHELEWA KUWASILISHA MICHANGO WCF

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe.Prof.Joyce Ndalichako akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mkutano wa ofisi za WCF leo Jijini Dar es Salaam. Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe.Prof.Joyce Ndalichako akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mkutano wa ofisi za WCF leo Jijini Dar es Salaam. Mwakilishi wa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw. Joseph Nganga akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe.Prof.Joyce Ndalichako uliofanyika katika ukumbi wa mkutano wa ofisi za WCF leo Jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. John Mduma akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano wa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe.Prof.Joyce Ndalichako uliofanyika katika ukumbi wa mkutano wa ofisi za WCF leo Jijini Dar es Salaam. Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe.Prof.Joyce Ndalichako (katikati) akiwa katika mkutano na waandishi wa habari katika ukumbi wa mkutano wa ofisi za WCF leo Jijini Dar es Salaam.Kulia kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. John Mduma na kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Huduma za Ajira (TaESA) Bw. Joseph Nganga ambaye alimwakilisha Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Watumishi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) wakimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe.Prof.Joyce Ndalichako akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mkutano wa ofisi za WCF leo Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

********************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

SERIKALI imetangaza msamaha wa riba kwa waajiri waliochelewa kuwasilisha michango katika Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) ambapo watakaonufaika na msamaha huo ni wale waliokwishalipa malimbikizo ya michango wanayodaiwa na Mfuko huo na wamebakiza deni la riba peke yake.

Ameyasema hayo leo Mei 5,2022 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe.Prof.Joyce Ndalichako wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mkutano wa ofisi za WCF Jijini Dar es Salaam.

Amesema hadi kufikia Agosti 2021 takribani waajiri 13,468 wa sekta ya Binafsi na waajiri 191 wa sekta ya Umma walikuwa kwenye orodha ya madeni ya riba.

"Kwa waajiri wote watakaolipa malimbikizo ya michango ya miezi ya nyuma wanayodaiwa na mfuko kabla ya tarehe 30 Juni 2022 nao pia watanufaika na msamaha huu wa ondoleo la riba ya michango kwa miezi tajwa". Amesema Prof.Ndalichako.

Pamoja na hayo amesema waajiri wote ambao hawajajisajili kwenye Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi watakapojisajili na kulipa michango stahiki inayodaiwa kabla ya tarehe 30 Juni 2022 nao pia watanufaika na msamaha wa riba ya malimbikizo ya madeni ya michango.

Nae Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Dkt. John Mduma amesema sualala kufutiwa kwa riba kwa waajiri waliochelewesha michango yao kwenye mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi ni kuwanodlea mzigo mkubwa waajiri hao ambapo walikuwa wanadaiwa kwa mujibu wa sheria.

Post a Comment

0 Comments