Ticker

6/recent/ticker-posts

TANGA UWASA KUWAPA MKATABA ULIOBORESHWA WAKAZI WA JIJI LA TANGA.

Ofisa Mahusiano wa Tanga Uwasa Devotha Mayala akiongea na waandishi wa habari juu ya mkataba walioboresha na kuwapatia wananchi ili kujua majukumu yao.************

Na Hamida Kamchalla, Tanga.

Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Tanga(Tanga Uwasa) imefanya maboresho ya mikataba yao na sasa wanaiwasilisha kwa wananchi ili wajue majukumu yaliyopo katika mamlaka hiyo katika kuhakikisha wananchi wanapata maji safi na salama.

Akiongea katika uzinduzi wa maonesho ya 9 ya biashara na utalii kwenye banda lao, Ofisa uhusiano wa Tanga Uwasa Devotha Mayala alisema wakazi wa jiji la Tanga wanaombwa kufika katika banda hilo ili wapate kujua huduma za maji zinavyotolewa kupitia mkataba wa huduma kwa wateja.
"Mwaka huu tunatumia maonyesho haya kuja kuwakabidhi watu mikataba ya huduma kwa mteja, tulifanya maboresho kwenye mkataba wetu tukiokuwa tunatumia sasa umeshakamilika na tunawakilisha kwa wateja wetu, ndani ya mkataba wa huduma kwa mteja tumeainisha Tanga Uwasa ni nini, inafanya nini, iko wapi na kwa sasa tunafanya huduma za kusambaza maji Tanga jiji, Muheza na Pangani" amesema MayalaAidha ameongeza kuwa katika banda lao wameweka huduma zote ambazo mwananchi ataweza kujua namna mchakato wa maji unavyofika mpaka nyumbani.


"Kwenye banda letu kuna wataalamu kutoka vitengo mbalimbali,huduma kwa wateja kama una maswali yeyote unaweza kupata majibu hapahapa" amesema Mayala.

Post a Comment

0 Comments