Ticker

6/recent/ticker-posts

TANZANIA RED CROSS SOCIETY- BARAZA LA VIJANA MKOA WA SONGWE***********

Mwenyekiti wa TRCS- Baraza la Vijana Mkoa wa Songwe Ndugu. Noel Mtafya amewaongoza Viongozi wa TRCS Baraza la Vijana Mkoa wa Songwe na Vijana wengine kutoka Mkoa wa Songwe ambao ni wanachama na volunteers wa TRCS katika maadhimisho ya miaka 60 ya kuanzishwa kwa Tanzania Red Cross Society yaliyofanyika tarehe 8 May jijini Dodoma.

Katika halfa hiyo walipata nafasi ya kupanda miti katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan katika kukabiliana na mabadiriko ya tabia ya nchi.

Pia, Mwenyekiti wa Baraza la Vijana, ambaye ni mjumbe wa mkutano mkuu, alishiriki Mkutano Mkuu tarehe 9 May, mbali na mambo mengine, alitumia nafasi hiyo kumpongeza Rais wa Tanzania Red Cross Society Mhe. David Mwakiposa Kihenzile (MB) kwa maono yake na uongozi wa mfano ambao kwa wakati wote umekua dira la wanachama na voluntia wote wa TRCS.

Aidha, Ndugu Noel Mtafya aliahidi kuwa, Baraz la Vijana -TRCS mkoa wa Songwe litaendelea kuwa kisaidizi namba moja cha serikali ndani ya Mkoa wa Songwe, ili kuifanya Songwe kuwa sehemu salama wakati wote.

“Red Cross Mahali Popote, Kwa Watu Wote”

Imetolewa na;

Emmanuel Chamba,

Katibu wa Baraza la Vijana- Tanzania Red Cross Society Mkoa wa Songwe

Post a Comment

0 Comments