Ticker

6/recent/ticker-posts

TBS YATAKIWA KUWEKEZA KATIKA VIFAA NA MIFUMO YA KIDIJITALI

Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Mhe.Kanali Denis Mwila akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza katika Maadhimisho ya Siku ya Vipimo Duniani yaliyofanyika leo Mei 20,2022 katika Ukumbi wa TMDA Jijini Mwanza.

Mkurugenzii Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania ((TBS), Dkt.Athuman Ngenya akizungumza Maadhimisho ya Siku ya Vipimo Duniani yaliyofanyika leo Mei 20,2022 katika Ukumbi wa TMDA Jijini Mwanza.


Baadhi ya washiriki wakiwa katika maadhimisho hayo mkoani mwanza

**********************

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limetakiwa kuwekeza katika vifaa na mifumo ya kidijitali ili kuendana na mapinduzi ya nne ya viwanda katika kuhakikisha ubora wa vipimo unaendelea kuthibitishwa na kuwajengea uweledi wafanyakazi wao na kuendana na mabadiliko hayo.

Ameyasema hayo Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Mhe.Kanali Denis Mwila akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza katika Maadhimisho ya Siku ya Vipimo Duniani yaliyofanyika leo Mei 20,2022 katika Ukumbi wa TMDA Jijini Mwanza.

Amesema kutokana na mapinduzi ya viwanda, mashine nyingi zinazofungwa katika viwanda vyetu zina teknolojia ya hali ya juu ya kidijitali hivyo hata namna ya upimaji au ugezi wa mashine hizo lazima ubadilike.

"Ugezi wa vifaa viwandani unaweza kufanyika kwa njia ya mtandao kwa kusafiirisha taarifa (data) kutoka TBS kwenda kwa mteja kwa kuunganisha mashine za kupima (reference standard ) na zile zinazopimwa (unit under test) kwa njia ya mtandao wa vitu (LoT) na kupata taarifa ya namna mashine hizo zinavyofanya kazi ". Amesema DC Mwila.

Pamoja na hayo DC Mwila amesema wanaoendesha mashine ama vifaa katika sehemu zao za kazi wanao wajibu mkubwa wa kujifunza na kuelewa vema teknolojia hiyo ya kidijitali ili waweze kuendesha na kutumia mashine na vifaa hivyo katika utekelezaji wa majukumu yao.

Post a Comment

0 Comments