Ticker

6/recent/ticker-posts

VIONGOZI WA DINI TUMIENI MAMLAKA YENU KUTOA ELIMU YA SENSA KWA WANANCHI

Kamisaa wa Sensa Spika wa Bunge Anna Makinda akizungumza na viongozi wa dini.

Baadhi ya viongozi wa dini walioshiriki Mkutano hio.

*************

Na Magrethy Katengu

Serikali imewaomba viongozi wa dini kutumia Mamlaka waliyo nayo kuelimisha waumini wao umuhimu wa kuhesabiwa ili kusaidia Bajeti ya serikali inapopangwa Serikali itambue namna ya kutoa huduma za kijamii.

Ombi hilo amelitoa Jana Jijini Dar es salaam Kamisaa wa Sensa Spika wa Bunge Mstaafu Mhe Anna Makinda katika kikao kazi na viongozi wa dini zote lengo likiwa ni kuzungumza nao na kuweka mikakati namna ya zoezi la kuhesabu watu na Makazi yao linafanikiwa kwani Serikili inatambua kuwa viongozi hao wanamchango mkubwa kwa watu kuhamasisha watu wasipuuzie kutoa taarifa zao sahihi kwa zitakapohitajika Kwa makarani.

"Tunawategemea sana viongozi wa dini zote kwani sisi sote tu waumini wenu hatuwezi kufanya Jambo lolote la kiserikali bila kuwashirikisha kwani tunatambua kuwa nyie mnaushawishi mkubwa kwa Jamii na mtu yeyote anapopata matatizo atahangaika lakini kimbilio lake kubwa ni katika nyumba za ibada hivyo tunawaomba mtusaidie katika hili'amesema Anna Makinda.

Hata hivyo amewasisitiza kuwahutubia waumini wao kutowafacha walemavu wakati wa zoezi Hilo na wawatoe ili nao taarifa zao zipatikane kwani nao kutokana na hali zao wanatakiwa wapatiwe huduma za kijamii Kwa namna ya pekee hivyo wakifichwa inakuwa vigumu kwa Serika kulaumiwa kuwa haiwajali huduma za jamii zinazotolewa ikiwemo afya shule siyo rafiki kwao

Naye Kamisaa wa Sensa upande wa Zanzibar Mohamed Hamnza amesema maandalizi yamekamilika Kwa asilimia 80 hivyo viongozi wa dini wanafahamu kuwa zoezi hilo kwao siyo geni hivyo watenge siku moja kitaifa kufanya ibada kuliombea jambo hilo liende katika amani na utulivu.

Naye Shkhe Issa Othama Issa amewahimiza waislamu wote kutambua kuwa zoezi la Sensa hata katika kitabu cha qurani tukufu imeandikwa juu ya umuhimu wa kuhesabu Sensa hivyo wajitokeze kwa wingi ili wahesabiwe

Kwa upande wake Askofu wa kanisa la Menonite Nelson Kisare amesema Sensa ni zoezi lilianzishwa na Mungu mwenyewe ukisoma katika kitabu cha biblia Hesabu 1:1-3 inaelezea jinsi Mungu anamugiza nabii Musa awahesabu wanawaizraeli awahesabu ajue idadi hivyo wataofanya juhudu kutoa elimu kwa waumini wote

"Waumini mtambue kuwa serikali haiwezi kupanga kutoa huduma kwa Jamii bila kujua idadi yao hivyo kila mmoja atoe taarifa sahihi kwani kuna usriri mkubwa hakuna mtu ambaye siri yake utatolewa"alisema Askofu Kisare

Naye Katibu wa Wachungaji Jimbo kuu kusini wa Tanzania (SEC ) Albat Nziku amesema hata wao katika kanisa lao Wana utaratibu wa kufanya Sensa hivyo zoezi Hilo kwa waumini wao halitakuwa geni na wameshaanza kuwahamasisha kupitia vyombo vyao vya habari Hope channel TV Monstar redio Gazeti la sauti kuu

Aidha,Makinda amewataka viongozi wa Dini katika kuhamasisha kazi ya sensa wanatakiwa kupandika matangazo mbalimbali ya sensa ili waamini waweze kupata elimu nzuri kuhusu sensa.

Post a Comment

0 Comments