Ticker

6/recent/ticker-posts

VITUO VITATU VYA KUTOA HUDUMA ZA AFYA VYASITISHWA KUTOA HUDUMA MKOANI KAGERA


Msajili wa Bodi ya Hospitali Binafsi Dkt.Francis Mwanisi akiongea na wamiliki wa hospitali binafsi wa Mkoa wa Kagera wakati wa kikao cha mrejeaho baada ya ukaguzi wa vituo vya kutolea huduma za afya binafsi mkoani hapo

Baadhi ya wamiliki wa hospitali binafsi walioshiriki kikao cha pamoja na bodi hiyo kutoka Wizara ya Afya.

Wamiliki wa hospitali binafsi wa Mkoa wa Kagera wakifuatilia ushauri uliotolewa na msajili wa Bodi.

Wamiliki wa hospitali binafsi Mkoani Kagera wakiwa kwwnye kikao mara baada ya ukaguzi uliofanywa na Bodi ya Hospitali Binafsi

Wamiliki wakisikiliza kwa makini sheria,kanuni na miongozo ya kuendesha vituo binafsi vya kutolea huduma za afya nchiniMmoja wa wamiliki akiuliza swali wakati wa kikao cha mrejesho mara baada ya ukaguzi

***********************

Na.Said Nyahoza,WAF-Kagera

Vituo vitatu vya kutolea huduma za afya binafsi vimesitishwa kutoa huduma na vingine 25 vimepewa adhabu Mkoa Kagera kufuatia ukaguzi ulofanywa na Bodi ya hospitali binafsi.

Vituo hivyo vya binafsi vimepata adhabu kufuatia ukaguzi ulofanywa na Wizara ya Afya kupitia Bodi ya Ushauri ya Hospitali Binafsi.

Akiongea wakati wa kikao cha pamoja kati ya Bodi na wamiliki wa hospitali binafsi Msajili wa Bodi hiyo Dkt. Francis Mwanisi amesema kati ya vituo 67 vilivyokaguliwa, vituo 25 sawa na asilimia 41.8 vimepewa adhabu na vingine vitatu kusitishiwa huduma mpaka watakaporekebisha mapungufu yaliyobainisha

Dkt. Mwanisi amemewataka wamiliki wa hospitali binafsi nchini kufuata sheria, kanuni na miongozo ya serikali ili kutoa huduma za afya zenye ubora katika vituo vyao

"Vituo vilivyo sitishiwa huduma vilikutwa na makosa yaliyoshindwa kuvumilika hii ni kusema kuwa bado vituo vingi havizingatii sheria, kanuni na miongozo vilivyosajiliwa nayo, hivyo nichukue fursa hii kuwataka wamiliki na watumishi wa hospitali binafsi kufuata sheria, kanuni na miongozo ili kutoa huduma bora kwa wananchi " Amesema Dkt. Mwanisi

Aidha,Dkt. Mwanisi amevitaka vituo binafsi vya Afya kutoa huduma kuendana na hali yao ya usajili na sio vinginevyo

"Baadhi ya vituo vinatoa huduma nje ya wigo wao wa usajili mfano; Zahanati kulaza wagonjwa zaidi ya masaa 24 kuwa na vitanda vingi zaidi ya vitanda 40 vya kulaza wagonjwa Dkt.Mwanisi

Vilevile Dkt. Mwanisi amewataka wamiliki wa hospitali binafsi kulipa mishahara ya watumishi wao kwa wakati ili waweze kutoa huduma kwa wagonjwa bila mawazo na kwa ufanisi wa hali ya juu

"Mshahara ni haki ya mtumishi, Baadhi ya Wamiliki wa Vituo binafsi vya kutolea huduma za afya hawalipi Watumishi wao mishahara kwa wakati kwani wengine hadi miezi sita, sijui unategemea ataishije" Amesema Dkt. Mwanisi

Dkt. Mwanisi ameongeza kuwa katika ukaguzi huo bodi ya hospitali binafsi nchini imebaini udhaifu na changamoto mbali mbali zilizopo katika vituo hivyo ikiwa ni Baadhi ya Vituo kutumia dawa zilizoisha muda wake wa matumizi ambazo ni sumu na vingine kuwa na Miundombinu mibovu ambayo inahatarisha Maisha ya Wagonjwa na Wafanyakazi kwa ujumla kwani baadhi ya majengo yana nyufa"

Post a Comment

0 Comments