Ticker

6/recent/ticker-posts

WIZARA YA AFYA KUANZA UTOAJI CHANJO YA POLIO AWAMU YA PILI MEI 18-21 MWAKA HUU.*************************

Na Emmanuel Kawau

Wizara ya Afya nchini inatarajia utoaji wa Chanjo ya Virusi vya Polio zaidi ya kwa watoto Milioni Kumi na Laki Tano walio chini ya Umri wa Miaka Mitano Nchini nzima,ifikapo Tarehe 18 Hadi 21 Mwezi huu, ikiwa ni Awamu ya Pili ya Kampeni ya Kutoa Chanjo hiyo.

Akizungumza Jijini Dar es salaam katika Semina kwa Waandishi wa Habari kuhusu Kampeni ya Utoaji Chanjo ya Polio Nchini, Afisa Programu kutoka Wizara ya Afya Kitengo Cha Mpango wa Taifa wa Chanjo Lotalis Robert Gadau ambapo Amesema Chanjo hiyo itatolewa Nyumba kwa Nyumba ambapo Katika Awamu ya Kwanza iliyofanyika katika Mkoa wa Songwe, Mbeya, Njombe na Ruvuma zaidi ya Watoto Million Moja walipatiwa Chanjo hiyo.

Hata Hivyo amesema Ugonjwa Huo huwapata watu wa Rika zote na hauna Tiba na Pale mtoto mtoto anapopatwa na ugonjwa huo hupata ulemavu wa gafla kwa miguu kuwa tepetepe na kushindwa kufanyakazi ama kufariki.

"Mzazi/mlezi mwenye mtoto chini ya umri wa miaka mitano anatakiwa kumwandaa mtoto wake kwaajili ya kupatiwa chanjo itakayomwongezea kinga mtoto ya kupambana na kirusi na baada ya kutoa chanjo mtoto atawekwa alama kwenye kidole cha mwisho ili wahakiki waweze kubaini watoto wangapi wamefikiwa na wangapi hawajafukiwa,” amesema Lotalis.

Naye.Mratibu wa Chanjo Katika Mkoa wa Dar es salaam Juma Haule amesema Katika Mkoa wa Dar es salaam unawatoto zaidi ya Watoto Laki Saba walio chini ya umri wa miaka mitano ambao wote wanatarajiwa kupatiwa chanjo hiyo.

Hivi karibu Shirika la Afya Duniani lilitangaza kupatikana Mtoto aliyekutwa na Virusi vya Ugonjwa Wa Polio katika Nchi ya Malawi ambapo kirusi hicho kinafanana na kirusi kilichopo Nchi ya Afghanistan na Pakistan hali inayosababisha Nchi zilizo jirani na Nchi ya Mawali kuanza kampeni ya kudhibiti usambaaji wa kirusi hicho.

Nchini Tanzania Mgonjwa wa Mwisho kupatikana na kirusi Cha Polio ni Mwaka 1996 amabae alikuwa mkoa wa Mtwara ambao mpaka hivi sasa Tanzania Haijapata kesi yoyote ya Kirusi hicho.

Post a Comment

0 Comments