Ticker

6/recent/ticker-posts

BARABARA YA HANDENI KUPITIA KIBIRASHI HADI MKOANI MANYARA KUTEKELEZWA.

Katibu wa Ccm Mkoa wa Tanga Suleimani Mzee Charasi akielekeza jambo kwa Mhandisi Zuhura Amani walipokagua barabara ya Handeni hadi Mziha, wilayani Handeni.
Wajumbe wa Bodi ya Barabara wakikagua ujenzi wa daraja wilayani Kilindi.
Msimamizi wa ujenzi kutoka TANROADS Mkoa wa Tanga Mhandisi Zuhura Amani akitoa taarifa ya mradi wa ujenzi wa daraja mbele ya Wajumbe wa Bodi ya Barabara wilayani Kilindi.
Mhandisi Zuhura Amani kushoto akijadiliana jambo na wajumbe hao, katikati ni Katibu wa Ccm Mkoa wa Tanga Suleimani Mzee Charasi



*******************
Na Hamida Kamchalla, TANGA.




SERIKALI kupitia Wakala wa Barabara nchini TANROADS mkoani Tanga imetenga kiasi cha zaidi ya sh bilioni 24 kwa ajili ya ujenzi wa barabara kuu inayounganisha Mikoa miwili ya Tanga na Manyara yenye km 88.89.


Barabara hiyo inayotarajiwa kujengwa kwa kiwango cha lami, inaunganisha Mikoa hiyo inapita katika Wilaya za Handeni na Kilindi mkoani Tanga, ilitokea Handeni mjini hadi Kiberashi na kufika katika mpaka wa Manyara.


Hayo yamebainishwa na Msimamizi wa Idara ya Ujenzi TANROADS mkoani Tanga Mhandisi Zuhura Amani wakati akitoa taarifa fupi ya miradi ya barabara mbele ya Wajumbe wa Bodi ya Barabara Mkoa wa Tanga iliyopo katika Wilaya hizo.


Amani amesema kazi za ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami inafanyika kwa awamu kulingana na fedha zilizotengwa na serikali.


"Awamu ya kwanza ya ujenzi ni sehemu ya Handeni hadi Mafuketa yenye urefu wa km 20 ambayo imeanza na Mkandarasi yuko kwenye maandalizi ya mwanzo ya kukusanya vifaa vya ujenzi na kutafuta eneo la kujenga kambi ya Mkandarasi na Mhandisi Msimamizi jwa ajili ya ujenzi huo" amesema.


"Lakini, taratibu za uwekaji wa alama za eneo la ujenzi wa barabara zinaendelea ili kubaini waathiriwa wa mradi huu kwa ajili ya kufanya tathimini na mradi huu utachukua miezi 24 ambapo miezi 12 ni kwa ajili ya uangalizi na muda wa mradi ni miezi 12" alifafanua Amani.


Aidha Mhandisi Amani amesema kuwa awamu ya pili ya ujenzi huo utaanzia Mafuleta hadi Kwediboma yenye urefu wa km 30 iko kwenye hatua za maandalizi ya kuandaa nyaraka za zabuni.


"Pia matengenezo mbalimbali yanaendelea kufanyika kila mwaka katika sehemu ya barabara ambayo haijafikiwa na ujenzi wa lami ili kufanya ipitike katika vipindi vyote vya mwaka kwa kutumia fedha zinazopangwa" amesema.


Naye Meneja wa Wakala wa Barabara za mijini na vijijini TARURA, halmashauri ya Wilaya ya Kilindi Mhandisi Martin Mwashambwa alisema wametekeleza na kukamilisha sehemu ya I'm 0.4 ya barabara ya katika kata ya Bokwa hadi Lengatei yenye jumla ya urefu wa km 5.1 kwa kiwango cha lami.


Amesema "madhumuni ya mradi huu ni kuwawezesha wananchi waishio maeneo haya ya kata ya Bokwa na kata jirani ya Songe kuboresha maeneo yao ya kiuchumi pamoja na kuongeza thamani ya viwanja, nyumba za makazi na biashara".


Mwashambwa amebainisha kwamba garama za utekelezaji wa mradi huo ni zaidi ya sh milioni 344.8 na mpaka sasa tayari zaidi ya sh my milioni 340.6 zimekwisha tumika huku alibainisha kazi mbalimbali zilizofanyika.

Post a Comment

0 Comments