Ticker

6/recent/ticker-posts

BODI YA KOROSHO YAPANIA KUTIMIZA LENGO, YATOA MABOMBA 14 YA KUPULIZIA DAWA.


**************************

Na Hamida Kamchalla, TANGA.


BODI ya Korosho nchini leo imekabidhi mabomba 14 ya kupulizia dawa kwenye mikorosho yenye thamani ya sh milioni 15.4 kwa Amcos za wakulima wa zao la korosho mkoani Tanga.
Wakati akikabidhi mabomba hayo kwa mkuu wa Mkoa wa Tanga Adam Malima, Kaimu Mkurugenzi mkuu Bodi ya Korosho nchini, Francis Alfred amesema wametekeleza agizo la mkuu wa Mkoa la kutaka kufufua mashamba pori ambapo pia Bodi iliona kwa asilimia kubwa katika mashamba hakuna mabomba ya kupulizia dawa.

"Sisi kama Bodi ya Korosho tumeangalia na kuona ni namna gani turaweza kuleta mabomba haya yatakayowasaidia wakulima wa korosho ili kusiwe na changamoto ya umwagiliaji wa dawa" amesema Alfred.

"Leo tumekuja kutekeleza kile ulichotuelekeza na tumekuja na mabomba 14 yenye thamani ya sh milioni 15.4 ambapo kila bomba moja thamani yake ni sh milioni 1.1, lakini kama tulivyosema tusitoe bure lazima kuwe na mchango fulani kwa yule anayepewa ili aone umuhimu wa kulifanya hili jambo" amebainisha.

"Kwahiyo kwenye mabomba haya, sisi Bodi tumelipia nusu ya garama ambayo ni sh milioni 7.7 na Chama cha Wakulima wa Korosho kulipia nusu ya garama, lengo ni kuhakikisha na wao wanagaramia" amesisitiza.

Post a Comment

0 Comments