Ticker

6/recent/ticker-posts

BRELA YAANIKA MAFANIKIO YA ONGEZEKO LA WATU KUSAJILI MAKAMPUNI KIPINDI RAIS SAMIA



*************************

WAKALA wa Usaji wa Biashara na Leseni Tanzania (BRELA) umesema kwamba wamekuwa na mafanikio makubwa ya ongezeko la mwitikio wa watu kusajili Makampuni,Majina ya Biashara sambamba na kupata leseni za biashara zao tokea Rais Samia Suluhu alipoingia madarakani.

Hayo yalisemwa na Msajili Msaidizi kutoka Brela Seleman Seleman wakati wa maonyesho ya 9 ya biashara na utalii yanayofanyika jijini Tanga ambapo wamekuwa wakitoa elimu juu ya umuhimu wa wananchi kusajili biashara zao.


Alisema kwamba kwa kipindi kimoja tokea Rais Samia aingie madarakani wameweza kusajili makampuni 11422 ambapo kwa najina ya biashara wameweza kusajili majina ya biashara 22251 lakini pia alama za biashara wamesajili 3056 ambapo katika leseni za kundi A wametoa leseni 12704.


“Kwa kipindi hiki kimoja cha mheshimiwa Rais wetu Samia Suluhu Hassan kimeonyesha mafanikio makubwa ukilinganisha na vipindi vingine jambo ambalo limeonyesha ari kwa watu kusajili makampuni, majina ya biashara lakini pia kupata leseni za biashara zao, “alisisitiza Seleman.


Aidha amesema kuwa hali hiyo pia imewaongezea ari wao kama watendaji wa Brela ambapo kupitia matamasha mbalimbali wanashiriki ili kuifikia jamii ambapo walengwa wakiwa wafanyabiashara wakubwa na wadogo.


“Wito wangu kwa wafanyabishara kabla ya kuanza kufanta jambo wawe wanapitia na kutafuta taarifa kwanza kwa wahusika ambao ni Brela kupitia mitandao ya kijamii au website zetu zinazoeleza sisi tunafanya nini na ikiwa kama kuna sehemu mtu hajaelewa kuna namba ya huduma kwa wateja hivyo watu wanaweza kupiga na kupata taarifa sahihi hii itawapunguzia wateja kupewa taarifa na watu ambao si sahihi, “alibainisha Seleman.

Wakizungumza katika banda hilo baadhi ya wakazi wa jiji la Tanga waliotembelea akiwemo Richard Otto alisema alilazimika kufika hapo ili aweza kujua namna ya kusajili jina la biashara na kampuni kwa kuwa alikuwa hajui umuhimu wa kusajili biashara yake.


Aidha alisema wanachonufaika nacho baada ya kufika hapa Brela ni kurasimisha biashara hasa kwa vijana ambao wamekuwa wakifanya biashara bila kusajili na hivyo kushindwa kutambulika.
“Tunashukuru tumepata suluhisho njia za kufanya mwanzoni huu mfumo ulikuwa unasumbua pale ulipoanzishwa mfumo wa usajili online lakini sasa ivi nimeambiwa taratibu zimekaa vizuri, “Alisema, Otto.


Hata hivyo kwa upande wake mkazi wa Korogwe ambaye alitembelea banda hilo Veronica Temu alieleza kufurahishwa na uwepo wa wakala huo kwenye maonyesho hayo kwamba utawasaidia kufanya usajili wa biashara zao ikiwemo kutumia simu yake au kompyuta akiwa nyumbani kwake na hivyo imewarahisishia kwa kiwango kikubwa.

Post a Comment

0 Comments