Ticker

6/recent/ticker-posts

DKT.SHEIN -AONGOZA KIKAO CHA KAMATI MAALUM.


MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Rais Mstaafu wa Zanzibar Mhe. Dk.Ali Mohamed Shein, akiongoza Kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar. kilichofanyika katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar.(kulia kwake) Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ambae ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, kikiwa ni Kikao cha kawaidi kilichofanyika leo 14-6-2022.(Picha na Ikulu)

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Rais Mstaafu wa Zanzibar Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein, (kulia kwake) Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ambae ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ,Mhe.Hemed Suleiman Abdulla wakiwa katika ukumbi wa mkutano Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar, baada ya kuwasili katika ukumbi kwa ajili ya Kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar, kilichofanyika leo 14-6-2022.(Picha na Ikulu)

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Rais Mstaafu wa Zanzibar Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein, akiongoza Kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar, kilichofanyika katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Unguja leo 14-6-2022,(kulia kwake) Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ambae ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Mhe. Hemed Suleiman Abdulla na (kushoto kwake) Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt.Abdalla Juma Sadala(Mabodi)(Picha na Ikulu)

******************************

NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.

MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein,leo ameongoza Kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Zanzibar.

Kikao hicho kimefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Afisi Kuu ya CCM,Kisiwandui Zanzibar.

Pamoja na mambo mengine Kikao kitapokea na kujadili Taarifa mbali mbali kutoka katika Idara na Vitengo vya Chama Cha Mapinduzi Zanzibar.

Kikao kilikuwa cha kawaida kwa mujibu wa matakwa ya Katiba ya Chama Cha Mapinduzi.

Viongozi mbali mbali walioudhuria kikao hicho ni pamoja Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla.

Wengine ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa ambaye pia ni Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe.Zubeil Ali Maulid pamoja na Wajumbe wengine wa Kamati Kuu ya CCM Taifa na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Zanzibar.

Post a Comment

0 Comments