Ticker

6/recent/ticker-posts

SERIKALI YA UGANDA YAIPATIA TANZANIA TUZO KUFANIKISHA MRADI WA EACOP


Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC Dkt Jamesi Mataragio akizungumza mara baada ya kupokea tuzo kutoka Mamlaka ya Uwekezaji nchini Uganda (Uganda Investment Authority-UIA) kwa kutambua mchango wa TPDC.

***************

Na Magrethy Katengu

Serikali ya Uganda imeishukuru Serikali ya Tanzania kwa kuendelea kudumisha ushirikiano wa masuala ya kiuchumi kwa uwekezajiwa wa mradi wa EACOP itakayosaidia watu kupata fursa za ajira baina ya nchi zote mbili.

Shukrani hizo zimetolewa leo Dar es salaam na Mratibu mradi wa EACOP Green economy UIA Bryan Bwana wakati hafla ya kukabidhi tuzo ya heshima kwa Shirika la Maendeleo iloyotolewa na Serikali hiyo kupitia Mamlaka ya Uwekezaji nchini Uganda (Uganda Investment Authority-UIA) lengo ni kutambua mchango wake kufikia maamuzi ya mwisho (Final Investment Decision) ya Uwekezaji mradi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi la Afrika Mashariki (EACOP).

"Waswahili wanasema "mcheza kwao hutunzwa"hili linajidhihirisha hapa leo ambapo tuzo hii inatolewa kwa TPDC kutambua mchango wake wa kitaalam katika kufanikisha Utekelezaji wa mradi wa EACOP"alisema Bryan

Sambamba na hayo amesema mradi huo umepitia katika hatua kadhaa za maamuzi ambayo yalifanyika kwa kuangalia mambo mbalimbali ikiwemo sheria sera za uwekezajiwa pamoja na uzoefu wa nchi na taasisi zake na TPDC ikiwa mstari wa mbele mafanikio yanapatikana katika mradi huo.

Naye Mkurugenzi Mtendaji Shirika la Maendeleo ya Petrol Tanzania(TPDC) Dkt Jamesi Mataragio ameishukuru Mamlaka ya Uwekezaji Uganda kwa kutoa tuzo kutambua mchango wa Serikali kupitia TPDC katika ushiriki wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki (EACOP)

Aidha TPDC Ina uzoefu katika kusimamia ujenzi wa miundombinu ya mafuta na gesi na wamekuwa na mchango wa thamani ya kipekee katika majadiliano na hata wakati huu ambapo mradi wa EACOP uko katika hatua za Utekelezaji.

Post a Comment

0 Comments