Ticker

6/recent/ticker-posts

TANZANIA NA CHINA KUSHIRIKIANA KUKUZA TEHAMA


Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mheshimiwa Nape Moses Nnauye (Mb.) akiagana na Balozi wa China nchini Tanzania Mheshimiwa Chen Mingjian mara baada ya kuhitimisha mazungumzo yanayolenga kujenga uwezo wa ukuzaji TEHAMA nchini; Mkutano huo ulifanyika Jumatano tarehe 15 Juni, 2022 jijini Dar es salaam.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mheshimiwa Nape Moses Nnauye (Mb.) akiagana na mgeni wake Balozi wa China nchini Tanzania Mheshimiwa Chen Mingjian muda mfupi baada ya kuhitimisha mazungumzo yaliyolenga kujenga uwezo wa ukuzaji TEHAMA nchini; mkutano huo ulifanyika Jumatano tarehe 15 Juni, 2022 jijini Dar es salaam.Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mheshimiwa Nape Moses Nnauye (Mb.) akipokea utambulisho wa wasaidizi wa Balozi wa China nchini Tanzania Mheshimiwa Chen Mingjian wakati alipokutana nae kwa mazungumzo. Mazungumzo yalilenga kutazama maeneo ya ushirikiano ili kujenga uwezo wa ukuzaji TEHAMA nchini; mkutano huo ulifanyika Jumatano tarehe 15 Juni, 2022 jijini Dar es salaam. Picha: TCRAWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mheshimiwa Nape Moses Nnauye (Mb.) akisisitiza jambo mbele ya Balozi wa China nchini Tanzania Mheshimiwa Chen Mingjian wakati wawili hao walipokutana kwa mazungumzo yanayolenga kujenga uwezo wa ukuzaji TEHAMA nchini; Mkutano huo ulifanyika Jumatano tarehe 15 Juni, 2022 jijini Dar es salaam

**************

Na Mwandishi Wetu

Tanzania na China zimekubaliana kuendelea kushirikiana katika kukuza usambaza wa TEHAMA nchini ili kuhakikisha azma ya Serikali kujenga Uchumi wa Kidijitali inafikiwa.

Makubaliano hayo ya ushirikiano yamefikiwa baina ya Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mheshimiwa Nape Moses Nnauye wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa China nchini Tanzania Mheshimiwa Chen Mingjian mkutano uliofanyika jijini Dar es salaa.

Kuhusu kupeleka huduma za mawasiliano maeneo yasiyofikiwa hasa maeneo ya vijijini China imekubali kuwa itaendelea kushirikiana na Tanzania ili kuhakikisha lengo hilo linafikiwa.

“Tutaendelea kuwahamasisha wawekezaji wa sekta ya mawasiliano nchini Kwetu ili waweze kufikisha huduma za mawasiliano kama ambavyo umeeleza” alitoa hakikisho Balozi Ke katika kikao chake na Waziri Nape.

Pamoja na kukubali kwamba suala la usalama mtandaoni linazo changamoto lukuki ambapo China imekuwa ikikabiliana nazo kila uchao Balozi Ke amesisitiza kuwa China bado inaona umuhimu wa kushirikiana na Tanzania ili kuhakikisha usalama mtandaoni unakuwa wa uhakika kwa kuweka mazingira na Miundombinu itakayowezesha Tanzania kukabili majanga ya kimtandao.

“Kimsingi tumekubaliana kuboresha zaidi suala la usalama mtandaoni hasa kwenye eneo la capacity building (kujenga uwezo) kwa wataalam wetu wa TEHAMA, kubadilishana programu za kiteknolojia zitakazowezesha ukuzaji wa sekta mtambuka za maendeleo kiuchumi kwa mfano kilimo, afya, biashara mtandao nakadhalika” alibainisha Waziri Nape.

Katika mkutano huo pande hizo mbili pia zimekubaliana namna zitakavyowezesha Tanzania kupokea na kukuza teknolojia mpya za mawasiliano ikiwemo Teknolojia ya mawasiliano ya kasi ya 5G.

Ili kuhakikisha Wizara inatekeleza majukumu yake hasa kupitia Idara ya Habari-Maelezo pande hizo mbili zimekubaliana kuboresha Miundombinu ya Idara hiyo itakayowezesha kuongeza ufanisi wa utoaji huduma, hasa kwa kuzingatia kuwa Idara hiyo inahusika kutoa taarifa mbalimbali za Serikali kwa wananchi.

Kuhusu uungwaji mkono katika Ujumbe wa Baraza-Tendaji la Shirika la Mawasiliano Duniani ITU ambapo Tanzania mwaka huu inawania kuchaguliwa tena kuingia kwenye Baraza hilo katika Mkutano Mkuu wa ITU unaotarajiwa mwezi Septemba baadae mwaka huu, China imekubali kuwa itaiunga mkono Tanzania, ikitumia fursa hiyo kuomba Tanzania pia iiunge mkono katika Nafasi mbalimbali inazowania.

Balozi Ke ametoa hakikisho kuwa atafikisha ujumbe pia kwa nchi nyingine Rafiki kuiunga mkono Tanzania kuwania Nafasi hiyo ambayo itashuhudia nchi 13 za Afrika zikichaguliwa katika nafasi za ITU katika mkutano wa jijini Bucharest nchini Romania utakaoketi Septemba na Oktoba mwaka huu.

Mara baada ya mkutano huo pande za wataalamu kutoka pande mbili za makubaliano zitaketi na kuja na mpango thabiti wa ushirikiano ili utekelezaji uanze mara moja

Post a Comment

0 Comments