Ticker

6/recent/ticker-posts

WAAFRIKA WATAKIWA KUWA WAMOJA KUJIKOMBOA KIUCHUMI

Baadhi ya Wawasilishaji wa Mada wakiwasilisha Mada kwenye kongamano la 13 la Kigoda cha Mwalimu Nyerere llinaloendelea Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo lilifunguliwa jana na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Rais Mstaafu Dkt.Jakaya Kikwete. Baadhi ya wadau wakifuatilia mdahalo kwenye kongamano la 13 la Kigoda cha Mwalimu Nyerere llinaloendelea Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo lilifunguliwa jana na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Rais Mstaafu Dkt.Jakaya Kikwete..

****************************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

MATUMAINI ya baadae ni kwamba Ukombozi wa Afrika ambao umekuwa ukizungumziwa enzi na enzi toka kwa wabigania uhuru kwa maana ukombozi kamili haujatimia na hauwezi kupatiikana iikiwa Afrika hawatakuwa wamoja.

Hayo yameelzwa leo Juni 9,2022 katika mdahalo kwenye kongamano la 13 la Kigoda cha Mwalimu Nyerere llinaloendelea Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo lilifunguliwa jana na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Rais Mstaafu Dkt.Jakaya Kikwete.

Akizungumza na waandishi wa habari katika tukio hilo, Mhadhiri Mwanadamizi, idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala wa Umma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt.Ng'wanza Kamata amesema Afrika ipo katika mapambano ya Ukombozi wa bara na yameelekezwa zaidi katika suala zima kujikomboa kiuchumi.

"Afrika ipate uhuru wake kiuchumi ambao haujaupata na iweze kumiriki na kutumia rasirimali zake kwaajili ya watu wake". Amesema Dkt.Kamata

Aidha amesema waafrika wanatakiwa kuwa wamoja kwani kuna waafrika ambao wanaishi Afrika na kuna waafrika ambao wanaishi nje ya bara la Afrika hivyo basi wakiwa wamoja utegemee kuona bara linakombolewa.

Post a Comment

0 Comments