Ticker

6/recent/ticker-posts

WAZIRI PINDI CHANA AKAGUA MAENDELEO YA MIRADI KIJIJI CHA MSOMELA.

Waziri Pindi Chana akiwasili katika uwanja mdogo wa ndege wa Mombo, kushoto ni mkuu wa Mkoa wa Tanga Adam Malima.
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Tanga ikiwa imejipanga kusalimiana na Waziri huyo.
Waziri akielekeza jambo kwa mkuu wa Mkoa.
Waziri akipita kuwasiliana na kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Adam Malima akisalimiana na mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege.
Mkuu wa Mkoa akitoa maelezo kwa Waziri Pindi Chana

*********************************

Na Hamida Kamchalla, HANDENI.


WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Pindi Chana ametembelea na kukagua maendeleo ya mradi wa makazi ya kudumu ya jamii ya wafugaji kutoka Ngorongoro, yanazojengwa katika kijiji cha Msomera, wilayani Handeni mkoani Tanga.

Katika ziara hiyo amekagua mradi wa maji ambao utawekewa tanki la lita laki moja na nusu na utahudumia kaya 400, ikiwa ni pamoja na shule za msingi na sekondari lakini pia kukagua nyumba za makazi hayo.

Akizungumza katika ziara hiyo, Waziri huyo amesema miundombinu imekamilika hivyo kilichonaki ma wananchi hao kutoka Ngorongoro kuweza kuhamia huku akisisitiza kwamba makazi hayo yamekamilika hivyo kuwasihi wananchi hao kuweza kuhamia kwa hiyari.

Post a Comment

0 Comments