Ticker

6/recent/ticker-posts

ASSEMBLY INSURANCE YAMTANGAZA NANDY BALOZI WAO


**************************

MSANII wa Bongofleva Faustine Charles "Nandy" amelamba ubalozi yeye pamoja na mtoto wake atakapozaliwa Huku akizima minong'ono ya swala la Afya yake na kupanda stejini kutumbuiza katika Tamasha la "Nandy Festival" linalotarajiwa kufanyika julai 23 uwanja wa Majimaji Songea Mkoani Ruvuma.

Akizungumza wakati wa kutambulishwa rasmi kuwa Balozi wa Kampuni ya Huduma za kibima "Assembly insurance" Meneja Maendeleo ya kibiashara Mwamvita Said meneja Kampuni hiyo inalenga kuwagusa watu wote na pia Huduma kubwa zaidi ya wakina mama wajawazito pamoja na mtoto atakaezaliwa pia kutokana na Msanii huyo alivyo na ushawishi mkubwa kwenye jamii kutokana na kazi zake Kampuni imeamua kujidhatiti na kubeba jukumu la kuhakikisha anajifungua salama na anarudi katika Majukumu yake ya Kila siku kupitia Bima ya Assembly.

Nandy amesema usalama wake kwenye Tamasha lake "Nandy Festival" ni asiilimia 100 kwa kuwa Kampuni hiyo itahakikisha anafanya show ,ikiwa tayari madaktari wamejiridhisha kuwa yeye na mtoto alieko tumboni Afya yao Iko salama zaidi.

" Wengi wameshangaa au wamekua wakijiuliza itakuaje Nandy anafanya show akiwa katika Hali ya ujauzito ,hapana kuwa mjamzito haimaanishi kuwa ubweteke ni muhimu kufanya mazoezi ya hapa na pale inasaidia kuimarisha Afya ya mama na mtoto Kwa ujumla hivyo katika kuhakikisha hilo Kampuni ya "Assembly insurance" ipo sanjari na Afya yangu na itahakikisha lolote la kiafya likitokea basi usalama wangu upo juu Yao Kwa Kila kitu kuanzia vipimo,usafiri wa haraka kufika hospitali na matibabu mengine."

Post a Comment

0 Comments